Kuhusu mashamba ya mimea tiba iringa si kwa ajili ya viwanda vyote bali ni makubaliano ya kibiashara ya kilimo cha mimea tiba baina ya kiwanda husika na wanaolima hayo mazao hususan katika utengenezwaji wa dawa za mseto za malaria zinazojulikana kama ALU n.k. Dawa ya mseto kuna ambazo zinatengenezwa China na huwa China wanalima wenyewe ila pia India wanatengeza dawa hizo pia.
Kuhusu malighafi za dawa ndio huwa imported kutegemeana na dawa husika inayotengenezwa, soko lake, sehemu inapotoka n.k
Kuna misitu na uoto wa asili sehemu kubwa katika maeneo yanayotuzunguka, mfano hata hapo ulipo umezungukwa na mimea tiba pia, kwa Tanzania kuna misitu Tabora, Kilimanjaro, Katavi n.k . pia ndani ya hifadhi za misitu na misitu mbali mbali ya jamii. Mapori unayoyaona Bagamoyo, mkuranga na mengineyo yote yana mimea tiba.
Nguvu kazi inayotumika kukusanya mimea hiyo ni kupitia wakulima maalum wenye elimu za dawa au makampuni, taasisi za tiba za asili kama za muhimbili n.k
Eneo hili la ukusanyaji wa malighafi lina fursa nzuri ya kutengeneza fedha.
Misitu huwa inakwisha kutokana na changamoto za mazingira, mabadiliko ya tabia nchi, ukame, ongezeko la idadi ya watu, majanga kama ukame, moto n.k pia kuongezeka kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji zinachangia sana misitu kuisha au uharibifu wa misitu na hifadhi.
Kutokana na hili la uharibifu wa misitu, utengenezaji wa dawa pia hutumia teknolojia kutengeneza dawa kwa kutumia kemikali na njia nyingine badala ya kutegemeana mimea tiba pekee kuhusiana na demand na supply