Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikiria Ndg. Elia Mwambo (45) Mkazi Mkazi wa Ngaramtoni Arusha kwa tuhuma za kusafirisha Dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Mirungi yenye uzito wa 187 kg.
Akitoa taarifa hiyo kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha ACP. Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasafirisha madawa hayo maeneo ya Ngaramton kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.793 CYU aina ya Carina.
Kamanda Madeni amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya usafirishaji wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali jijini Arusha.
Aidha mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya kulitolea maamuzi kisheria.