SoC02 Dawa za kulevya na athari zake katika maisha

SoC02 Dawa za kulevya na athari zake katika maisha

Stories of Change - 2022 Competition

Princely G

New Member
Joined
Aug 15, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Andiko langu litakua na sehemu tatu kuu, sehemu ya kwanza dawa za kulevya na maana yake. Sehemu ya pili urahibu wa dawa za kulevya na athali zake. Sehemu ya tatu namna ya kuepukanana na hili janga.

DAWA ZA KULEVYA.
Dawa za kulevya ni aina ya kemikali zitumikazo katika mwili wa mwanadam kwa matumizi mbali mbali pasina maelekezo ya dakitali ambazo mara baada ya kuingia mwili husababisha madhara makubwa hasa katika ubongo.kuna sababu kadha wa kadha zinazowasukuma vijana wengi ambao ni waoga wa maisha na changamoto zake kuangukia kwenye matumizi ya dawa hizi mfano ni ugumu wa maisha kuongezeka kwa majukum angali kipato kidogo, maumivu ya mapenzi au kuondokewa na mtu ambae unadhani ndie nguzo katika maisha na makundi. Mfano wa dawa za kulevya ni Kokeini, Heloini, Bangi mirra, Tumbaku na Pombe.

URAHIBU WA DAWA ZA KULEVYA NA ATHALI ZAKE KATIKA JAMII.
Urahibu wa dawa za kulevya hutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi hatari hali inayomfanya mtumiaji kubadilika na kushindwa kufanya shunghuli zake za kawaida bila ya kemikali hizo, hii humfanya kubadilika kimatendo hisia na muonekano tofauti kabisa na jamii inayomzunguka wengine huwa vibaka na wezi kutoka na kua dhoofu kimwili na kushindwa kufanya shuli yoyote ya kimaendeleo hivyo ili wajipatie japo pesa ya kununua dawa hizo wanaamua kua wezi na vibaka mitaani mfano panya road wengine huishia kupiga debe katika vituo vya daradara jijini Dar es Salaam.

F95F0112-0485-4892-A093-694EF78D9C65.jpeg

Picha kutoka soba house Dodoma.

JE NINI KIFANYIKE.
Janga la dawa za kulevya linaenea kwa kasi sana ulimwenguni sababu ni biashara yenye pesa nyingi sana na iliyoshikiliwa na watu wenyenguvu kubwa duniani.

Hivyo ikwa upatikanaji wa kemikali hizi utaangamia biashara hii itakua kama mtoto yatima asiejua wapi pakuelekea. Pia wahusika wakuu wa nyumba za kupata nafuu maarufu kama soba house wanapaswa kujitafakari upya tena kwa makini sana.

NB: Kinacho angamia ni kizazi kipya tegemeo la kesho.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom