MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,267
Yametimia.Kesi ndio inakua kubwa sana hapo hawezi kuchomoka kabisa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yametimia.Kesi ndio inakua kubwa sana hapo hawezi kuchomoka kabisa.
======
Sakata la Madawa ya Kulevya limechukua sura mpya kufuatia mwanadada mashuhuri Wema Sepetu, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa, kutoa ya moyoni juu ya sakata zima la kukamatwa kwao na kuhusisha tukio hilo na hila dhidi yake.
Pamoja na mambo mengine, Wema amedai kwamba RC Paul Makonda anatembea na Agnes Masogange na amempangia nyumba Makongo ndio maana hajakamatwa ktk kadhia ya Dawa za Kulevya.
Operesheni ya kukamata wanaojihusisha na madawa ya kulevya ilianzishwa na Paul Makonda mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo alitaja majina ya watu mbalimbali wanaohitajika kituoni kwa ajili ya mahojiano, wakiwemo wasanii na maaskari polisi.
=====
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Simon Sirro amesema kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wa Dawa za Kulevya 112 na jumla ya kete 299 huku 12 kati yao wakifikishwa Mahakamani.
Kwa taarifa hii soma > Makonda: Watuhumiwa madawa ya kulevya kuanza kupandishwa kizimbani leo au kesho
Who the hell is mkuu wa mkoa?? Trump anasemwa ndo iwe huyo mkuu wa mkoa??nimefurahi sana maana anajiongezea kesi juu ya kesi,anamtukana mkuu wa mkoa? hajui kuwa anamtukana pia raisi,muache apumzike jela tu.
Umethibitishaje kama walishaachaUkweli wanajichanganya wenyewe, kama ulijua anauza madawa kwanini usimtaje. Vyombo vya dola hakuna?
Si ulihojiwa je ulimtaja, sasa ukitaja ukirekodiwa ndiyo mahakama?.
Hadi hapo ushaanza kuonekana ni mfwa maji asiyeisha kutapatapa Wema, gugumaji utashikilia hata ukiona povu la wimbi utatamani ulidake uokokea na kifo cha maji.
Hata ikisemwa kuwa Aness aliwahi kukamatwa na madawa huko Bondeni, ile ni miaka imeenda kama unaamini ni kweii pia haiwezi kumuweka ndani. Unaweza kukuta alishaacha, utamtaja vipi hapo? Ni sawa kumuorodhesha Ray C au Young Dee hivi sasa kwenye list wakati walishaacha kitambo
Hahahaaaaa,buku 7 tu inatosha!Buku 2 rent,buku 5 fee!Ila ukichelewa unagongewa mlango,yaani nikishagongewaga mzigo ndio kwanza unarudi hata kama ulikuwa karibuNipo njiani naelekea buguruni kwenye mambo yetu.
Mshamba utamjua tuu! Ukuu wa mkoa ni cheo cha msimu walikuwepo kina magesa mulongo na walivuma haswa wako wapi leo? acheni kutukuza ujinga hata kama elimu hamna.nimefurahi sana maana anajiongezea kesi juu ya kesi,anamtukana mkuu wa mkoa? hajui kuwa anamtukana pia raisi,muache apumzike jela tu.
Ndugu,
Tujiulize swali kidogo,wakati watuhumiwa wa matuzi ya madawa ya kulevya na watumiaji ambao wengi wameshikiliwa toka ijumaa wakifikishwa leo mahakamani.
Ni nini kilichotokea kwa wema sepetu?
Mbona katika orodha ya waliopewa dhamana jina lake limo lakini hakuwepo mahakamani.
Kwa nini wema sepetu hakufikishwa mahakamani?
pia kwa maelezo ya kamanda siro jana alitoa ufafanuzi kwa kila mtuhumiwa na alidai kwamba walipoenda kwa wema sepetu kumsachi walipata msokoto wa bangi na karatasi zinazotumika kwenye bangi.
Lakini pia ikumbukwe kwamba wema sepetu aliitwa kuripoti polisi na hakukamatiwa nyumbani na kosa aliloitiwa polisi lilikuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya kabla ya kubadilishwa na kutuhumiwa kuwa muuzaji kwa mujibu wa maelezo yake kwenye clip inayotembea mitandaoni toka jana,sasa nina swali,
Hivi mtu anayetuhumiwa kutumia madawa ya kulevya inawezekana kweli akaitwa polisi kujieleza kwa kosa hilo huku akiacha madaw ya kulevya ndani kwake?
Aliyewanyima watanzania elimu ndiye aliyeliangamiza taifa la tanzania.
JF mods najua hampendi nyuzi zangu ila huu muuache.
Swelana.