'Dawa za kuongeza nguvuza kiume sasa tishio Z'bar'

'Dawa za kuongeza nguvuza kiume sasa tishio Z'bar'

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, ameshangazwa na wimbi la uuzaji wa dawa za nguvu za kiume uliojitokeza katika maeneo ya misikiti visiwani humu.
Akifunga mjadala kuhusu ripoti ya Kamati ya Maendelo na Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto ya mwaka 2012/2013 , Duni alisema waganga wamevamia maeneo ya misikiti na kuuza dawa za kienyeji zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Duni alisema inashangaza kuna dawa zinazouzwa na za wanaume pekee lakini akasema ni jukumu la wananchi wenyewe kuwa makini kwa vile siyo kila daktari wa tiba asilia anaweza kutibu kila aina ya maradhi.
Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, vyombo vya habari vimekuwa vikichangia kuwaingiza wananchi katika matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa ubora wake kutokana na kutangaza bila kupata ukweli wa dawa hizo.
Alisema baadhi ya dawa zinazouzwa huchangia matatizo ya wagonjwa kutokana na kuzitumia bila maelekezo ya kitaalam, hivyo wanapozidiwa na kwenda hospitali, ugonjwa huwa mkubwa na wenginekupoteza maisha.
Hata hivyo, Duni alisema ataendeleakusimamia ukweli kwa vile umri wake unafikia ukingoni.
Alisema serikali imeshatunga Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira namba11 ya mwaka 2012 ambayo itasaidiakuondoa matatizo ya matumizi mabaya ya tiba asilia.
CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom