Dawa za mswaki sio rafiki kwako, fanya maamuzi magumu

Kwamhuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2014
Posts
1,762
Reaction score
401
Nimejiwekea tabia ya kutokula au kutofanya chochote kwa kuwa nimemuona mtu fulani akila kitu hicho na labda akakisifia kwamba ni kizuri.Na pia kutofanya jambo lolote kwa kuwa tu eti nimemuona mtu akifanya jambo hilo.

Basi leo asubuhi nilichukua mswaki wangu ili nisafishe meno,nikakumbuka kwamba sijawahi kuchunguza kwa makini tooth paste ambayo natumia,yaani Colgate Herbal, imetengenezwa kwa kutumia vitu gani.

Nilipoisoma,niligundua kwamba chini ya neno Colgate kuna viandishi vidogo vinavyosomeka"Fluororide toothpaste."Sikuishia hapo, nikachunguza zaidi,nikaenda kwenye "active ingridients."

Nikakuta kwamba kitu kimojawapo ambacho paste yangu imetengenezewa kinaitwa Sodium Monofluorophosphate,kiasi chake kikiwa 1.1% tu.Nikajiuliza swali, vitu vingine vilivyotumika kutengeneza dawa yangu ni nini, maana hii 1.1% ndio ile Fluoride,sasa 98.9% ni nini?

Kwa kukisia nikasema lazima kutakuwa na maji,sasa vitu vingine ni nini,na mbona havikuandikwa.Na kwanini havikuandikwa.Frankly nilistuka nikaanza kufanyia utafiti paste yangu nikianzia na vile vitu ambavyo vimeandika nikianzia na Fluoride.

Katika utafiti wangu, niligundua kwamba paste ya mswaki inatengenezwa kwa kutumia vitu vifuatavyo:-

Active ingridients>1.Sodium Fluoride 0.24%

2. Triclosan 0.30%;Inactive ingridients>1.Hydrated Silica

2. Water

3. Glycerin

4. Sorbitol 5.PVM/MA Copolymer

6. Sodium Lauryl Sulphate

7. Cellulose Gum

8. Flavour

9. Sodium Hydroxide

10. Carrageenan

11. Propylene Glycol

12.Aspartame/Sodium saccharin

13.Titanium Dioxide.Ukichunguza hivyo vitu,utagundua kwamba kuna kitu cha kuleta ladha kama ya karafuu hivi(Flavour).Sina hakika hicho ni kitu gani, kwa hiyo kuna alama ya kuuliza hapo.

Kwanini haikusemwa wazi hiyo flavour ni kitu gani.Kuna jambo gani linafichwa?Nimechunguza makemikali yote tajwa na nimegundua kwamba makemikali mengi yaliyotajwa hapo juu yana madhara kwetu na mengi yana madhara ya muda mrefu,kwa hiyo si busara kununua madawa ya miswaki bila kuyasoma na kujua vitu vilivyotumika kutengeneza madawa hayo.

Si busara pia kuamini kwamba makampuni yanayotengeza dawa hizo yanajali afya yako,mara nyingi sio kweli.Kosa hili linaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa afya yako.

Nitazungumzia makemikali machache yaliyotajwa kama ifuatavvyo:

1. Sodium Fluoride-Wanaojiita wataalam wa meno kwa muda mrefu wamedai kwamba kemikali hii inazuia meno kuoza.Wanasema inajenga meno imara na yenye afya.

Ukweli hata hivyo ni kwamba Sodium Fluoride ambayo ni matokeo ya uzalishaji wa Aluminium viwandani inatumika pia kwenye dawa za panya na dawa za kuua wadudu.Kumeza 1/10 ya aunsi ya fluoride inaweza kuua mtu mzima mwenye paundi 100.Kula kiasi kidogo cha Fluoride kinaweza kikaleta kizunguzungu,kutapika na kuharisha.

Ni ajabu kwamba pamoja na ubaya wake,Fluoride bado inaendelea kutumika kwenye utengenezaji wa dawa za meno!

2. Sodium Lauryl Sulfate-Kemikali hii inatumika pia kutengenezea dawa za wadudu na inaaminika kwamba ni kisababishi cha kansa mbalimbali.

3. Triclosan-Kemikali hii inapunguza kiwango cha homoni ya thyroid mwilini ambayo kazi yake ni kuufanya mwili utumie chakula vizuri(metabolism) na inaweza pia kuwafanya bakteria wawe sugu kwa madawa ya aina ya antibiotics.

4. Aspartame-Kemikali hii kazi yake ni kuleta ladha ya sukari.Hata hivyo ukweli ni kwamba hii ndiyo kemikali ya hatari kuliko zote, zinazotumika kutengeneza vitu vinavyoliwa na wanadamu.

Kemikali hii iko kwenye vinywaji vinavyodaiwa kwamba havina sukari.Hata hivyo aspartame ina uwezo wa kuleta kisukari,kuongeza uzito,cancer,ugumba,kupoteza kumbukumbu,matatizo ya neva.

Wenyewe wanasema ujio wa aspartame ni kama kupanga upya viti ndani ya Titanic.Aspartame ni tamu mara mia mbili zaidi ya sukari ya kawaida kwa hiyo ni sio ghali kutumia.

Kwa kemikali hizo chache itoshe kukujulisha kwamba dawa za meno sio rafiki kwako.Ndio maana katika dawa yangu ya meno watoto chini ya miaka 6 wana kiwango chao cha kutumia, tena kwa kusimamiwa na dawa isimezwe,kitu ambacho hakiwezekani.Kwa watu wazima vivyo hivyo, dawa isimezwe na mdomo usuzwe vizuri baada ya kutumia.

Tahadhari zote hizi zinaonyesha kwamba dawa hizi si rafiki kwetu.Uamuzi ni wako.Labda kuna haja ya kurejea Eden.
 
We utaishi milele?? Tumia dawa uwe nameno safi acha uoga we unataka uishi miaka mingapi sasa
 
OK...Safi kabisa vp kuhusu ingredints zilizo kwenye white dent? Na umalizie ni nin tufanye kama m-badala wa hayo sasa
 
Kufa ni lazima ndio,lakini I want to die a natural death,not otherwise.Na kuwa na meno safi sio hoja,kwa kuwa unaweza kutengeneza at home dawa ya mswaki ambayo haina makemikali hayo ya sumu na ikafanya meno yako kuwa safi na imara.
We utaishi milele?? Tumia dawa uwe nameno safi acha uoga we unataka uishi miaka mingapi sasa
 
Kufa ni lazima ndio,lakini I want to die a natural death,not otherwise.Na kuwa na meno safi sio hoja,kwa kuwa unaweza kutengeneza at home dawa ya mswaki ambayo haina makemikali hayo ya sumu na ikafanya meno yako kuwa safi na imara.
naomba kujua jinsi ya kutengeneza
 
Kufa ni lazima ndio,lakini I want to die a natural death,not otherwise.Na kuwa na meno safi sio hoja,kwa kuwa unaweza kutengeneza at home dawa ya mswaki ambayo haina makemikali hayo ya sumu na ikafanya meno yako kuwa safi na imara.
Help us on how to make alternative tooth paste at home.
 
Sina choyo mkuu.Tengeneza dawa yako ya mswaki kwa kutumia ingridients zifuatazo:1.vijiko sita vya mafuta ya nazi mazuri 2.Vijiko sita vya baking powder nzuri 3.Matone 25 ya mafuta ya mkaratusi au grapefruit 4.Kijiko kimoja cha unga wa stevia.Stevia ni mmea ambao ukipondwa unatumika kama sugar substitute.Stevia inatumika pia kwenye vidonda vya moto,maumivu ya tumbo na wakati mwingine inatumika kama contraceptive.Changanya vitu vyote vizuri kwenye chombo mpaka upate rangi ya cream.Weka kwenye kichupa kisichoingiza hewa kwa urahisi na funga vizuri tayari kwa kutumia itakapo hitajika.
naomba kujua jinsi ya kutengeneza
 
Basi tutarudi kule kwenye midaha na majani ya mmbaazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…