Bora mkuu umeleta uzi wa meno hapa, binafsi ni muhanga wa matatizo ya meno na niliamua kufuatilia baadhi ya taratibu za mafunzo ya kinywa.
utafiti ulio ufanya hapa mzuri kabisa, halafu wadau niwaambie haijalishi ni dawa gani unayoiweka kwenye meno yako bado ni hatari, ndani ya kinywa kuna natural bacteria ambao wanabalance mabo yote ya kinywa na kukinga kinywa na maambukizi mbalimbali, matumizi mkubwa ya madawa hatimaye huua hao bacteria jambo linaloweza kuleta madhara.
Kingine utashangaa watu wanaamka asubuhi wanapiga mswaki wakati hajala chochote unajiuliza anaondoa nini sasa? wengi wanaopiga mswaki asubuhi kabla ya kula hawapigi mswaki kabla ya kulala na hivyo midomo yao hutoa harufu.
iko hivi, wale bacteria wanakula mabaki ya chakula kwa sababu umeyaacha hujayaondoa na hivyo wakijisaidia ndio maana mdomo wako unakuwa na harufu, na wanapokula hayo mabaki ndipo wanaweza hata kuleta madhara kwenye meno na kinywa kwa ujumla.
kingine hawa bacteria wanakuwa active sana wakati mtu amelala unapokuwa upo active wao wanakuwa wanafanya kazi pole pole sana, ukilala tu ndo wanashambulia na ndiyo maana asubuhi unaamka mdomo unanuka kwa sababu ya by-products za activities zilizokuwa zinaendelea. kwa hiyo muda muhimu saana wa kupiga mswaki kuliko yote ni usiku kabla ya kulala, na utagundua utaamuka na kinywa fresh hakina harufu hauna haja ya kupiga mswaki kabla ya chai. Piga mswaki baada ya chai ondoa mabaki usitembee nayo.
kitu kingine kuhusiana na hayo madawa ya meno, kinacho sababisha watu wapate magonjwa ya meno au harufu ni interplay ya bacteria na mabaki ya chakula, kwa hiyo ukiwa na namna ya kuondoa mabaki ya chakula kinywani bila kuweka extra madawa utakuwa umezuia madhara makubwa. Dawa nyingi za meno zina chemichals ambazo ni strange and hazardous kwa natural process za mwili, nashauri tupunguze matumizi ya madawa ya mswaki (hayo ni madawa hatuumwi) mara nyingi tumia tu mswaki na maji ondoa mabaki ya chakula kinywani inatosha. tumia dawa ya mswaki kwa nadra. ikiwezekana basi mwarobaini ni mzuri zaidi.
watalaam pia wanatuambia kuwa kunavitamini K ambayo inapatikana kinywani pale mtu anapo amka na hivyo kwenda kupiga mswaki na kutema kila kitu ni kuitokomeza hautaipata. njia ya kuipata ni kunywa maji asubuhi au kula chochote asububuhi kabla ya kupiga mswaki.