Dawa za mswaki sio rafiki kwako, fanya maamuzi magumu

Ya forever living inatengenezwaje yenyewe mkuu?
 
Hayo mambo ya dawa ya meno tuyaache kwanza, huyu dr slaa anadhani watanzania hatujielewi kabisa hatuwezi kufanya political analysis, au alitaka yeye apeperushe bendela ya ukawa?
 
NILIKUWA NATAFAKARI JUMBE HIZI MBILI.MOJA NI HII YA DAWA YAMENO LENGO LA MTOA MADA NI LIPI? PILI UJUMBE WA DR SLAA. LENGO LAKE NI LIPI? KUWA KILA MTU ALIYE CCM HAFAI HATA AKITOKA? AU LENGO NIKUTUAMBIA LOWASA HAFAI? na vipi kuhusu magufuli mbona haja mgusia kabisa.
 

Watanzania wana akir sana ndo maana dr slaa hakupewa nchi mwaka 2010,
 
Ndugu jiulize swali dogo tu. "Kwa nin unatumia dawa ya meno chemichalised halaf baada ya muda jino linauma mpaka inafikia hatua ya kuling'oa"?
 
umejitahidi kuandika vizuri. lakini unapaswa kuelewa tukisena kemikali flani ni sumu haimaanishi hata kiwango kidogo hakikubariki. vitu vingi unavyotumia kila siku ni sumu au vina madhara pale vinapozidi viwango vinavyokubalika. hata mwanga wa jua una utra violed radiations ambayo ikiwa kwa kiasi kinacho kubalika inasaidia mwili kutengeneza vitamin D, lakini ikizidi husababisha kansa ya ngozi. point yangu ni kwamba hizo ingridients za colgate ziko kwa vipimo vinavyokubalika kwa matumizi ya binadamu. ukitaka kuishi namna hiyo hutaweza kula wala kunywa chochote kwakua hakuna kitu safe kwa100% duniani na ndio maana watu hawaishi milele. kila kitu kina madhara ndio maana kuna kufa.
 
Kuanzia leo narud kwenye mti, kuna ndugu yangu alinikataza kutumia dawa za mswaki kuwa zinamdhara lakini sikumuamin
 
Mwishowe lazima ung'oke meno tu mkuu, utumie dawa usitumie ukibogoyo huuepuki labda uzee uwe msamiati kwako.
 
Hiyo number 2 sodium laurly sulphate inapatikana pia kwenye cleaning material kwenye shampoo na hata sabuni nyingi za kuogea
 
Bora mkuu umeleta uzi wa meno hapa, binafsi ni muhanga wa matatizo ya meno na niliamua kufuatilia baadhi ya taratibu za mafunzo ya kinywa.
utafiti ulio ufanya hapa mzuri kabisa, halafu wadau niwaambie haijalishi ni dawa gani unayoiweka kwenye meno yako bado ni hatari, ndani ya kinywa kuna natural bacteria ambao wanabalance mabo yote ya kinywa na kukinga kinywa na maambukizi mbalimbali, matumizi mkubwa ya madawa hatimaye huua hao bacteria jambo linaloweza kuleta madhara.
Kingine utashangaa watu wanaamka asubuhi wanapiga mswaki wakati hajala chochote unajiuliza anaondoa nini sasa? wengi wanaopiga mswaki asubuhi kabla ya kula hawapigi mswaki kabla ya kulala na hivyo midomo yao hutoa harufu.

iko hivi, wale bacteria wanakula mabaki ya chakula kwa sababu umeyaacha hujayaondoa na hivyo wakijisaidia ndio maana mdomo wako unakuwa na harufu, na wanapokula hayo mabaki ndipo wanaweza hata kuleta madhara kwenye meno na kinywa kwa ujumla.
kingine hawa bacteria wanakuwa active sana wakati mtu amelala unapokuwa upo active wao wanakuwa wanafanya kazi pole pole sana, ukilala tu ndo wanashambulia na ndiyo maana asubuhi unaamka mdomo unanuka kwa sababu ya by-products za activities zilizokuwa zinaendelea. kwa hiyo muda muhimu saana wa kupiga mswaki kuliko yote ni usiku kabla ya kulala, na utagundua utaamuka na kinywa fresh hakina harufu hauna haja ya kupiga mswaki kabla ya chai. Piga mswaki baada ya chai ondoa mabaki usitembee nayo.
kitu kingine kuhusiana na hayo madawa ya meno, kinacho sababisha watu wapate magonjwa ya meno au harufu ni interplay ya bacteria na mabaki ya chakula, kwa hiyo ukiwa na namna ya kuondoa mabaki ya chakula kinywani bila kuweka extra madawa utakuwa umezuia madhara makubwa. Dawa nyingi za meno zina chemichals ambazo ni strange and hazardous kwa natural process za mwili, nashauri tupunguze matumizi ya madawa ya mswaki (hayo ni madawa hatuumwi) mara nyingi tumia tu mswaki na maji ondoa mabaki ya chakula kinywani inatosha. tumia dawa ya mswaki kwa nadra. ikiwezekana basi mwarobaini ni mzuri zaidi.
watalaam pia wanatuambia kuwa kunavitamini K ambayo inapatikana kinywani pale mtu anapo amka na hivyo kwenda kupiga mswaki na kutema kila kitu ni kuitokomeza hautaipata. njia ya kuipata ni kunywa maji asubuhi au kula chochote asububuhi kabla ya kupiga mswaki.
 
Kati ya dawa za mswaki na kuingia uvinza, ipi ni hatari zaid?
 
Mimi naomba kuuliza kama kuna madhara yanayoweza kutokea kama mtu kwa makusudi au bahati mbaya atameza maji yaliyochanganyikana na dawa ya meno kwa muda mrefu kama mwaka mmoja hivi?
Nauliza hivyo kwa sababu nina mwanafamilia wangu ambae miaka miwili iliyopita aling'oa meno mawili ya nyuma. Baada ya kama miezi tisa hivi kila anapopiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno anahisi kichefuchefu na hali hiyo kupelekea kutaka kama kutapika na hivyo sehemu ya maji yanayokuwa bado kinywani kushuka kooni huku yakiwa na sehemu ya hiyo dawa ya mswaki. Hali hii imedumu kwa takribani mwaka mmoja na utokea pale tu anapopiga mswaki kwa kutumia dawa na asipotumia dawa tatizo linakuwa halipo.Tulimshauri abadili aina ya dawa na akafanya hivyo lakini tatizo bado liko palepale. Kwa wenye uelewa je ni nini inaweza kuwa imesababisha hali hii na pia ni yapi madhara ya kumeza dawa hizi kwa kipindi kirefu kama hicho? Je umezaji wa dawa hizo hauwezi kuathiri mapafu na kuleta matatizo kama pneumonia n.k?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…