Mkuu...
Kwanza hongera sana kwa jinsi ulivyokuwa na udadisi mkubwa kuhusiana na masuala ya kutengeneza dawa...
Ila idea yako ni nzuri sema ipo kinadharia sanaa na kimatendo hiko kitu hakiwezekani kufanyika...
Utengenezaji wa dawa ni sayansi na hivyo basi ina misingi yake... Nadhani kuna mdau hapo juu ametangulia kukueleza kuhusiana na vitu kama "preservatives", "excipients", "binders" na kadhalika.
Katika kada ya Ufamasia kuna somo linaitwa PHARMACEUTIC... Hili huwa lina dili na kuandaa fomula za dawa kwaajili ya matumizi ya dawa kwa kuzingatia maumbile ya mwanadamu kibaiolojia na kikemikali...
Sio kila dawa inatakiwa iwe kidonge, unga unga, au kimiminika.. Inategemea na hali ya ugonjwa na mgonjwa husika..
Kiufupi tu huwezi kutengeneza dawa kwa kutumia leaflet na Google pekee.. Inahitajika uwe na ufahamu zaidi ya hapo.
Nimeanza kutafuta njia ya kutengeneza dawa kwa matumizi binafsi kitambo kidogo. Nikapata njia ambazo sikuzipenda.
Njia zenyewe ni:
1: TIBA LISHE
Nilikuwa nafocus kwenye nutrients (virutubisho) vinavyotibu ugonjwa fulani, nikishavipata, naangalia chakula gani chenye nutrients hizo kwa wingi. Nikaona kama itanipotezea muda wa kila siku kununua vyakula.
2: KUZIZOEA NUTRIENTS AUTOMATICALLY KWA LADHA
Nikawa natumia chakula chenye nutrient fulani kwa wingi kuizoea na kuikariri ladha ya nutrient fulani ili hata nikila chakula kingine, nitambue hiki chakula kina nutrient fulani. Nikatumia kanuni ya certain taste = certain nutrient. Hii nayo ikanishinda.
3: DIGESTION SYSTEM
Nikajiuliza, baada ya chakula kusagwa, ni kiungo gani kinasambaza nutrients kwenda sehemu mbalimbali za mwili, ingawaje baadaye nilipata jibu, yaani 'villi', lakini haikunisaidia, niliishia kujua neno villi tu basi.
4: CHEMICAL REACTION YA VYAKULA TOFAUTI
Nikawa nachukua vyakula viwili tofauti halafu najiuliza nikichanganya ladha itaniletea nutrient ipi?, nikaona hapa ndiyo kabisa nitapoteza muda, kemia yenyewe nilikimbia shuleni.
5: JIBU LIMEPATIKANA
Nikaona hapa nikitumia maarifa yangu kupata njia ya kutengeneza dawa, nitafeli, nikaamua kutumia mgongo wa dawa za hospitali, nikaanza kuchambua kila ingredients, nikawa naona maruweruwe ya maneno ya Kigiriki na Kilatini.
Baadaye nikaona hapa nikichambua kila ingredient nitapoteza muda, nikapata wazo la kutumia ingredients zote kwa pamoja, ambalo ndiyo jibu sasa.
Tukija kwenye maoni yako, mimi nasema inawezekana, kwasababu kazi yangu itakuwa siyo kubuni, kutunga forumula, wala kufikiria kisayansi, kazi yangu itakuwa ni kucopy na kupaste ingredients ambazo wanasayansi wameshazifanyia kazi tayari.