DAWASA: Chemba ya maji taka iliyokuwa inamwaga maji ya taka Ilala sokoni, imetengenezwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
DAWASA Wametengeneza Chemba iliyokuwa inamwaga maji taka Ilala Sokoni.

Awali Mdau wa JamiiForums.com alisema, "Hali ya mtaa wa tabora na uhuru ni mbovu sana kutokana na chemba ya maji taka kuziba na kutiririsha maji taka yenye kinyesi barabarani ambapo wafanyabiashara wa soko la mbogamboga na matunda ILALA hupanga bidhaa zao. Cha ajabu eneo hili lipo mkabala kabisa na zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam na mkuu wa wilaya ya Ilala."

Akatoa Wito DAWASA washughulikie kero hiyo.

Akiongea kuhusuana na hilo tatizo,
Everlasting Lyaro, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano DAWASA amesema, "Kazi ya uzibuaji na usafishaji wa line ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa imekamilika. Changamoto ya kuziba kwa line hizo ni utupaji ovyo wa taka katika chemba za Majitaka na taka hizo ni kama vile Nguo kukuu, mifuko, chupa, mifuko ya kubebea bidhaa, taulo za kike ambazo mafundi wetu walizikuta kwenye chemba."

DAWASA imetoa wito kwa Wananchi kuheshimu miundombinu hii ya Majitaka na kuacha kutupa taka ngumu ili kutunza miundominu hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…