A
Anonymous
Guest
Mimi ni mtumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Kumekuwepo na changamoto ya kukosekana kwa usawa na haki katika upandishaji wa madaraja na mabadiliko ya majukumu kwa watumishi, kinyume na miongozo ya utumishi wa umma.
Kwa mfano, kuna watumishi ambao wamebadilishiwa majukumu bila kuwepo uwazi kuhusu vigezo vilivyotumika kufanya maamuzi hayo. Wakati huo huo, kuna watumishi wengine wenye sifa na vigezo vinavyofanana au hata kuzidi vya wenzao, lakini hawajapewa fursa hizo. Vilevile, wapo watumishi wengi ambao kwa muda waliotumikia katika nafasi zao wanastahili kupandishwa madaraja, lakini hadi sasa hawajapandishwa, ilhali wenzao waliotumikia kwa kipindi kifupi zaidi wamepandishwa.
Hali hii imekuwa ikiwavunja moyo watumishi, inapunguza ari ya kufanya kazi, inashusha morali kazini na kuibua hisia za kutotendewa haki miongoni mwa wafanyakazi.
Tunaiomba Wizara ya Maji pamoja na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuchunguza suala hili na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha taratibu za upandishaji wa madaraja na ugawaji wa majukumu zinafanyika kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia miongozo ya utumishi.