JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kuna huu mchongo ambao unaendelea Kibaha japo kuna washkaji zangu nilizungumza nao wanadai kuwa siyo Kibaha peke yake bali maeneo mengi.
Inadaiwa kuwa wana mchezo wa kubambikia watu bili za maji.
Inashangaza kidogo kwa kuwa malipo unalipia online, waoa wanafaidikaje hapo au ni uzembe wao tu?
Kuna ndugu yangu mita yake ya maji imeharibika na ameshaenda mara kadhaa kuripoti lakini hawaendi kuibadilisha, kisha ikifika mwisho wa mwezi wanabuni bili wanakutumia.
Kuna mama mmoja naye nilimkuta palepale ofisini kwao Maili Moja analalamika kuwa kuna siku bili ilikuja zaidi ya elfu 60 kwa mwezi wakati bili yake huwa haizidi buku 15 kwa mwezi.
Wakamwambia mama fuatilia labda mabomba yako au system yako ya maji ina shida, bi mkubwa akakomaa hakufanya kitu anasema akalipa kishingo upande na hakurekebisha popote na matumizi yake ni yaleyale, mwezi uliofuata wakatuma bili buku 15 ileile ya mwanzo.
Mimi mwenyewe mita yangu imeharibika ina mwaka sasa, haisomi lakini kila mwezi jamaa wanakuja eti kusoma mita na bili natumiwa, nikumuuliza unasomaje hizo namba ananijibu niendi ofisini kwao ndiyo wana majibu.
Wazee hoo kitu ipoje huo kwenu?