DAWASA Kibamba wakaazi wa Malamba mawili hatupati maji, tumewakosea nini?

DAWASA Kibamba wakaazi wa Malamba mawili hatupati maji, tumewakosea nini?

Mbavu mbili

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
1,457
Reaction score
874
Licha ya kutumia gharama kubwa za kuvuta maji majumbani mwetu, WAKAZI WA MALAMBA MAWILI (zone 10) wamekuwa wakiishi kwenye mateso makubwa sana ya maji. Huduma hiyo haipatikani kabisa, wakati mwingine zaidi ya mwezi maji Huwa hayatoki. Unapowaailiana na injia wa maji na watendaji wamekuwa na majibu yasiyo na matumaini, majibu ya kutoa moyo yanayoumiza Wananchi.

Hata wanapoamua kutoa maji hutoa maji saa name za usiku Kwa masaa matatu tu. WAKAZI Walio kwenye miinuko ndiyo usiseme. Inafikirisha sana, mathalani mwezi huu maji hayajatoka, mwezi uliopita walifungua maji yasiyokuwa na presha Kwa masaa matatu au manne.

Tunamuomba Mheshimiwa Waziri wa maji atusaidie kwenye hili kwani awali hakukuwa na tatizo la maji kiasi hiki Kwa maana mradi ulipowafikia waakazi hao. Tuna Imani kubwa na Mh waziri wa maji, Kinachoshangaza zaidi eneo la kwembe, Ubungo na kinyerezi maji siyo tatizo.

Mwisho waongeze umakini kwenye kusoma mita za wateja, mara kadhaa makosa yamekuwa yakifangika Kwa kuletewa bili isiyoendana na matumizi inapotokea maji yakatoka .

Msaada kwenye hili, Wananchi wamechoka kununua maji Kwa gharama kubwa
 
Back
Top Bottom