DAWASA kununua mitambo yenye thamani ya bilioni 13 kuzalisha maji Ruvu juu

DAWASA kununua mitambo yenye thamani ya bilioni 13 kuzalisha maji Ruvu juu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam) inafanya ununuzi wa pampu nne zinazogharimu shilingi bilioni 13 kusaidia uzalishaji maji katika mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu uliopo mkoani Pwani.

Akizungumza leo Februari 27 Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhandisi Tyson Mkindi, baada ya ziara ya Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa kutoka Ubungo katika miradi ya DAWASA amesema “tupo katika mpango wa manunuzi ya pampu mpya kwa mtambo huu wa Ruvu Juu pampu nne ambazo gharama yake ni takribani bilioni 13 tunazidi kwenda kuongeza uzalishaji”

Mhandisi Mkindi amewatoa hofu wananchi wa Ubungo na maeneo mengine yanayotegemea maji kutoka Ruvu Juu kuwa bado hali ya uzalishaji maji ni nzuri kutokana na kina cha mto Ruvu kuendelea kuwa rafiki kwa uzalishaji.

“kwa hali ya sasa ilivyo kuanzia mtoni kiwango cha maji ni hali nzuri level ya mto ni mita 17 ili uzalishaji usimame inatakiwa mita 14 au chini mto wetu una maji ya kutosha”

Kwa upande wake Diwani wa Kimara Ismail Mvungi ziara hii imekuwa nafasi nzuri kwao kufikisha changamoto za maji zilizopo katika maeneo yao na pia kujua sababu za uwepo wa upungufu wa maji.

Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Ubungo, Sophia Fitina amesema sasa atakuwa na majibu kwa wananchi wake pindi watakapouliza juu ya uwepo wa mgao wa maji katika maeneo yao.

Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wametembelea mradi wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu na mradi wa kisasa wa kuchakata majitaka wa Kisopwa.

Chanzo: Jambo TV
 
🤔
giphy.gif
 
Back
Top Bottom