DAWASA: Kutakuwa na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kwa siku nne!

DAWASA: Kutakuwa na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kwa siku nne!

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Wakazi wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na upungufu wa huduma ya maji kwa siku nne kuanzia kesho Jumanne, Novemba 3 hadi 6, 2026, wakati Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) ikifanya matengenezo ya bomba kuu lenye kipenyo cha inchi 72 linalopokea maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Dawasa, Everlasting Lyaro, matengenezo hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha miundombinu ya majisafi ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Nino. Kutokana na matengenezo hayo, uzalishaji wa maji katika mtambo huo utapungua kwa asilimia 60 kwa kipindi cha saa 96, hali inayotarajiwa kuathiri upatikanaji wa huduma kwa wakazi wanaohudumiwa kupitia chanzo hicho.

Maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Zinga, Kiromo, Dunda, Kisutu, Magomeni, Nianjema, Fukayosi, Makurunge, Kerege, Mapinga, Mbweni, Mabopwepande, Bunju, Kunduchi, Kawe, Mbezi Juu, Goba, Wazo, Makongo, Kijitonyama, Kinondoni, Makumbusho, Msasani, Mzimuni, Tandale, Ndugumbi, Kigogo, Kariakoo, Mchikichini, Upanga Magharibi, Gerezani, Upanga Mashariki, Mchafukoge, Jangwani, Kivukoni, Ilala, Mnyamani, Liwiti, Kilungule, Kilakala, Mianzini, Keko, Kurasini, Miburani na Chang’ombe.

Dawasa imewaomba wateja na wananchi katika maeneo hayo kuvumilia usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa matengenezo hayo.

Pia, imewahimiza kupanga matumizi ya maji na kuhifadhi kiasi cha kutosha kwa matumizi muhimu kabla ya kazi kuanza ili kupunguza athari za upungufu wa huduma katika kipindi hicho.

Untitled-design-2022-02-21T125712.140.jpg
 
Sijuwi tucheke, tunune au tutukane?!
Watu hatuna maji bunju wiki 2!
Hawa DAWASA haki ya nani hatujuwi maofisini wanafanya kazi gani?! Cha kushangaza waweza pita mitaani hasa uswalihini ukakuta maji yanatiririka barabarani tu!
🤬😡😠😤
 
Ndugu Mteja, kutakuwa na upungufu wa maji kuanzia Jumanne, Novemba 3,2026 hadi Ijumaa, Novemba 6,2026
Sababu: Matengenezo ya bomba kubwa linalopokea Maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini. Maeneo ya Bunju hadi Ilala yataathirika.
DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

#MitanoTena#
 
Ukosefu wa maji NCHINI kwa masababu lukuki mpaka lini?!?!?!?! DAWASA Kuna bro yuko UK, aliingia 1994 Yuko mpaka leo 2026, anadai. HAIJAWAHI MAJI KUKOSEKANA HUKO! HAIJAWAHI UMEME KUKATIKAKATIKA BILA SABABU YA MSINGI! TUNAJIULIZA WENZETU WANAWEZA VIPI HUKU SISI TUNASHINDWA?!
Vyanzo vya maji kibao, jua kali sana, upepo mikoani hasa Ile mbaya, wakufunzi kibao. SHIDA NINI?! LABDA UWAJIBIKAJI, LABDA UVIVU, LABDA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA, LABDA UJINGA, LABDA .....
 
Back
Top Bottom