DAWASA Luguruni Kibamba tufungulieni maji kwa wakati, tumechoka kuteseka

DAWASA Luguruni Kibamba tufungulieni maji kwa wakati, tumechoka kuteseka

mwandende

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
11,005
Reaction score
20,805
HABARI WAKUU,

Kuna hili suala la Dawasa wilaya ya ubungo ,
tarafa ya kibamba,
kata ya kwembe,
mtaa Luguruni, Dare saalam.

Eneo hili limekuwa lina tatizo sugu la maji,
ambalo limetengenezwa na Dawasa wenyewe eneo hilo la Luguruni , lengo la kupiga pesa kwa njia ya kuuza maji,
kupitia kwenye Bomba la maji ya DAWASA (kibamba Kwa Mangi), pamoja na magari ya maji ya watu binafsi yanayofanya biashara hyo kwa miongo kadhaa sasa.

Miaka ya kuanzia 2000-2015 ,
eneo lote la kibamba kulikuwa hakuna maji ya bomba kwenye nyumba nyingi.,
Ikapelekea biashara ya kuuza maji kupitia magari mitaani kushamiri.

Magari yote yalikuwa yananunuwa maji ya bomba eneo la Dawasa kwa Mangi,
Ambapo lipo bomba kubwa la Dawasa.

Hapo Dawasa huuza maji kwa sh 2000 unit(litres1000) ,
Na hawa jamaa wa magari hutuuzia wanainchi kwa sh 15,000 kwa 1 unit.

Wanainchi hulazimika kununuwa units 3 kwa pamoja,
sababu wenye magari hawauzi 1 unit, (dumu 1 la litres 1000) wanauza kuanzia units 2 (dumu litres 2000)na kuendelea. ,

Yabidi mwanainchi kulipia sh 45,000 kwa units 3(dumu litres 3000) za maji ya bomba kutoka kwenye magari mitaani.

Mwaka 2016-2018 kulitandazwa mabomba ya mchina majumbani, wanainchi tukaanza kusahau shida ya maji ktk eneo hilo. Baada ya serikali kuleta mabomba majumbani.

Ikawa ndiyo mwisho wa biashara Ile ya Dawasa na magari ya maji mitaani..
Wengi wenye gari za maji yalibebea matofali au kugeukia biashara zingine.
Maji yalitoka kila nyumba tena ni masaa 24/7.

Kuna kipindi Dawasa walitaka kuleta janja janja ya kufunga baadhi ya mabomba ili wapate kuuza maji. Magufuli aliwashukia kama mwewe na kuwapa onyo.. Shida ya maji ilikoma.

Now 2022 baada ya kufariki Magufuli,
Shida ya maji imerudi kwa kasi ya ajabu.

Tatizo ni lile lile la kutengeneza shida ya maji.
Sasa wenye magari ya kuuza maji, wameyafufuwa tena.
Vurugu za magari ya maji zimeanza upya tena.
Wanachokifanya Dawasa,
ni kufunga baadhi ya mabomba yanayopeleka maji kwa wanainchi, Magari ya maji ya eneo hilo yaweze kuuza maji kwa kipindi hicho..

Na Dawasa wakiendelea kuuza maji kwa wingi ktk bomba lao hilo la kibamba kwa Mangi.
Haya yote yanafanywa kwa baraka zote za uongozi wa Dawasa luguruni kibamba, pamoja na engineers wao.
Yaani Africa sijuwi nani katuroga.

Maji yapo fully kisimani,
lakini yanafungwa kusudi ili wengine wateseke na wengine wajizidishie kipato kwa kuuza maji kwa bei juu kwa wanainchi ,

Wanainchi tukipiga Kelele Sana, Basi watafungulia maji usiku Sana, kuanzia 0100 am --0600 am,

Lengo ni kufunguliwa muda huo ili wengi wasipate nafasi ya kuchota maji na shida iwe pale pale.

Hivi tutaishije kwa kusubiri maji ya bomba mara 1 kwa mwezi? ,
Maji yanatoka mwezi hadi mwezi kweli na tupo mjini Daresalam? Tena wilayani kabisa?

Mbele ya uso wa mkuu wa wilaya ya ubungo tukose maji mwezi mzima, Kwa makusudi kabisa?

Yaani maji yapo lakini wanagoma kutufungulia kwa wakati sababu ya maslahi yao.

Kwa kweli Dawasa mnatutesa Sana kwa shida ya maji.
Njaa zenu pamoja na tamaa zenu za upigaji zisitupe wanainchi maisha magumu..

Kama ni kwl maji hayatoki,?au kuna matatizo yeyote? Je yale yanayotoka pale kwenye bomba lenu la Dawasa kibamba kwa Mangi yanatokea wapi?
Na kwann iwe mtaa wetu luguruni pekee?
Kama sio hujuma?na ufisadi? Ni nini? Kuna taarifa kuwa wanaohusika na kufungulia maji hupewa hongo na wenye magari ili kufunga maji.

Na hata hayo maji mnayouza hapo Dawasa bombani sidhani kama pesa zinafika serikalini..Kwa style mnayokwenda nayo,,
bila Shaka pesa zinaingia kwenye mifuko yenu. Dawasa mnatumia nguvu nyingi Sana kuendelea kufanikisha biashara hiyo ya yenu ya maji na magari ya maji huko mitaani. Ili wanainchi wateseke na kulazimika kununuwa maji kwa lazima.

Kama kwa siku Dawasa mnauza units 500 kwenye magari mitaani, Na kama pesa haziingii serikalini haiwezikuwa ni hujuma nzito kwenye shirika pamoja na serikali?

Tunaiomba serikali tukufu ya mama yetu raisi SSH walifuatilie hili. Kuna pesa zinapigwa kibamba kwa Mangi kwenye bomba la Dawasa.

Huku wanainchi wa kawaida wakiendelea kuteseka kwa shida ya maji ya kutengenezwa na uongozi wa Dawasa luguruni kibamba. Hawa ndy watu wachache wanaoipaka matope serikali na kuichonganisha na wanainchi wake.

Kama mbwai mbwai!
 
Miaka 60 ya uhuru CCM mmeshindwa ku supply maji mijini ambako population ni 20% tu. Je hali ikoje huko vijijini kwenye 80% ya watu wote nchini?
Maji yapo mkuu,, tatizo maji yanafungwa,.ili kutengeneza tatizo la shida ya maji,

Ili wauze maji ya kwenye magari.

Njaa mbaya sana.
 
Kwembe!nimekumbuka harakati za maisha mwaka 2009.

Nilitoka kwembe kwa mguu mpaka kimara suka kwa dingi.

Ndo nikaenda kuomba nauli kwa mama wa kufikia [emoji16][emoji16].

maisha hayaa
 
Ndio kusema mzee umeamka kuteka maji, ukaona upandishe na Uzi.
 
Kwembe!nimekumbuka harakati za maisha mwaka 2009.
Nilitoka kwembe kwa mguu mpaka kimara suka kwa dingi.
Ndo nikaenda kuomba nauli kwa mama wa kufikia [emoji16][emoji16].
maisha hayaa
Ukiishi maeneo hayo kama huna wa kukupa hata 1000 ukikwama.

Basi andhar kanoon inakuhusu mkuu.[emoji2][emoji2]

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Ndio kusema mzee umeamka kuteka maji, ukaona upandishe na Uzi.
[emoji2][emoji2][emoji2],

Hapa tulipo tuna week 3 maji hayatoki.

Unavizia maji kama unalinda ulinzi shirikishi.

Na kubambikia watu bili za pesa ndefu pia hawako nyuma.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Ni eneo gani huko, maeneo mengine maji yapo 24/7, Kata ya Kwembe ina maji ya kutosha kabisa..
 
Ni eneo gani huko, maeneo mengine maji yapo 24/7, Kata ya Kwembe ina maji ya kutosha kabisa..
Luguruni/ kibamba,,maeneo ya makondeko hadi kwa Gamba.

Eneo lote lipo kwenye biashara za kununuwa maji ya magari.

Tukipaza sauti Sana Sana wanafungulia maji kwa masaa 3 au manne Tu.
Tena usiku wa manane.
 
Luguruni/ kibamba,,maeneo ya makondeko hadi kwa Gamba.

Eneo lote lipo kwenye biashara za kununuwa maji ya magari.

Tukipaza sauti Sana Sana wanafungulia maji kwa masaa 3 au manne Tu.
Tena usiku wa manane.
Poleni aisee, maeneo ya kwa Mkuu wa Wilaya, ukishuka hadi kwa masister kuelekea Njeteni mambo ni [emoji91] maji 24/7.
 
Back
Top Bottom