KERO DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu salam,

Wakazi wa Mbezi Beach hatuna maji ni siku ya tatu sasa, kuna nini?

Au kuna matengenezo yalitangazwa na yamenipita? Maana sijasikia popote, hata kama kuna matengenezo ndio siku tatu jamani? Mnafikiri tunaishije?

Halafu maji hayajaacha kuwa na machafu/vumbi! Sasa vumbi kwenye maji haitoshi sasa mnatukatia kabisa! Na bado bili ikija inagonga mule mule!

Aloo mturudishe maji jamani, Aweso ulijitapa wakati wa kusoma bajeti kuwa sekta imeimarika, ndiyo hivi wanachi siku tatu hatuna maji? Na kuna nyuzi kibao humu za maji kuwa machafu, huyaoni haya malalamiko, ubora huo uliokuwa unaongelea ndio upi?

Turudishieni maji bwana!

===

Ufafanuzi wa DAWASA soma: DAWASA: Kuendelea kwa matengenezo ya umeme katika mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini
 
Wakuu salam,

Wakazi wa Mbezi Beach hatuna maji ni siku ya tatu sasa, kuna nini?

Au kuna matengenezo yalitangazwa na yamenipita? Maana sijasikia popote, hata kama kuna matengenezo ndio siku tatu jamani? Mnafikiri tunaishije?

Halafu maji hayajaacha kuwa na machafu/vumbi! Sasa vumbi kwenye maji haitoshi sasa mnatukatia kabisa! Na bado bili ikija inagonga mule mule!

Aloo mturudishe maji jamani, Aweso ulijitapa wakati wa kusoma bajeti kuwa sekta imeimarika, ndiyo hivi wanachi siku tatu hatuna maji? Na kuna nyuzi kibao humu za maji kuwa machafu, huyaoni haya malalamiko, ubora huo uliokuwa unaongelea ndio upi?

Turudishieni maji bwana!
Hawa jamaa hovyo sana, Leo ni siku ya nne, maji hayatoki, hakuna taarifa yoyote,
Ukipiga simu ofisini kwao Kawe hawapokei,
 
Hili ni tatizo la nchi nzima, kama vile hz mamlaka za maji na mawakala wa maji wameambiana watukomeshe wananchi

huduma za maji kila siku znakuwa mbaya kuliko awali

ngoja kipindupindu kitokee watu wafe, kwa kunywa na kutumia maji machafu
 
Back
Top Bottom