DAWASA na TANESCO kwanini hamzingatii ratiba?

DAWASA na TANESCO kwanini hamzingatii ratiba?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na kero kubwa ya kampuni za DAWASA na TANESCO kutoa ratiba ya kuwepo au kutokuwepo na huduma sehemu fulani kwa siku fulani lakini ukiifuata unaambulia patupu.

Makampuni haya yamekuwa yakiwapoteza watu mbalimbali kwa sababu ya kutoa ratiba zisizofuatwa. Siku chache zilizopita DAWASA wametoa ratiba ya mgawo wa maji Dar lakini kwa maeneo mengi ratiba ile haina uhalisia.

Ratiba inaweza kuonesha siku fulani eneo lako maji yatatoka lakini ukienda eneo hilo unakuta hola. Kwa upande wetu huku Kimara ni siku ya tano sasa maji hayajatoka.

Wakati mwingine bora msitoe ratiba ili tusiwe na matarajio yoyote.

Jitafakarini kwenye hili.
 
Kweli hawazingatii ratiba

Sijui walizitoa za nini
 
Salaam Wakuu,

Kumekuwa na kero kubwa ya kampuni za DAWASA na TANESCO kutoa ratiba ya kuwepo au kutokuwepo na huduma sehemu fulani kwa siku fulani lakini ukiifuata unaambulia patupu...
Huu mgao kuna maeneo tunao mwaka mzima, nadhan maji yakikatika maeneo ya serikali au viongozi ndio wanatangaza mgao, ila sisi since huu mwaka tuna mgao.

wajitafakari
 
Back
Top Bottom