DAWASA na TARURA warekebisha barabara zilizoharibiwa kutokana na mifumo ya Majitaka Mitaa ya Mbezi Beach

DAWASA na TARURA warekebisha barabara zilizoharibiwa kutokana na mifumo ya Majitaka Mitaa ya Mbezi Beach

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mrejesho wa Taarifa ya Jamii Forums

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kwa kushirikiana na Mkandarasi wa mradi wa Usafi wa Mazingira Mbezi Beach kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Ltd (BCEG) pamoja na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), leo Februari 10,2025 wamepitia barabara zilizorepotiwa kuharibika kutokana na mifumo ya Majitaka Mbezi Beach ambazo ni Mbezi Beach kwa Zena na Kanisani Road kwa ajili ya kuhakiki taarifa hizo.

Kwasasa barabara hzio zinapitika vizuri na kupitia picha mjengeo zilizoambatanishwa na taarifa hii kuonyesha barabara zinapitika.

Picha zilizotumika kwene taarifa ya awali ni za kipindi cha mvua kabla ya maboresho

Kazi mbalimbali zitaendelea kutekelezwa ili kuboresha barabara hizo ikiwa ni pamoja na kujaza vifusi vya udongo chemba zote na kushindilia Ili kuwezesha Magari kupita vizuri zaidi.

Everlasting Lyaro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
DAWASA

WhatsApp Image 2025-02-10 at 13.47.32_f12261c3.jpg

WhatsApp Image 2025-02-10 at 13.47.32_10b16079.jpg

Kusoma hoja ya awali, bofya hapa ~ Wanaoboresha mifumo ya majitaka Mbezi Beach (Dar) wanaacha barabara zikiwa zimefumuliwa ovyo, mvua zinakuja tutatafutana
 
Back
Top Bottom