DOKEZO DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!

DOKEZO DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Wakuu DAWASA leo naomba kuwafikishia malalamiko yangu kuhusu ubovu wa huduma zenu. Kuna shida ya Maji katika mitaa ya Tabata hasa kuanzia Posta kuelekea Segerea, Takriban Wiki 2 sasa Maji hayatoki na DAWASA hawatoi taarifa yoyote kueleza kama kuna uhaba wa Maji au Matengenezo yanafanyika.

Kuna wananchi wamejaribu kufika katika Ofisi zenu zilizopo Chama Segerea lakini mnawapa majibu yasiyoeleweka kwamba Maji yapo wakati kiuhalisia mtaani hakuna huduma ya Maji.

Ifike muda muwambie tu ukweli wananchi kwamba huduma imeshindikana au haipatikana ili watafute mbadala kuliko kukaa wanasubiri Maji kumbe kuna mgawo wa kimyakimya unaendelea na hamsemi.

Kuweni na utaratibu wa kuwapa watu taarifa wawe wanajiandaa kuwa kuhifadhi maji kwa tahadhari.

Majibu ya DAWASA, soma hapa: DAWASA yafafanua sababu ya maji kukatika mitaa ya Tabata

Soma zaid;
 
DAWASA wanafeli sana, Bonyokwa wiki ya tatu hakuna maji. Na bill zikitoka zinakuwa kubwa as if tulikuwa na maji.
 
Mbunge wenu anasemaje

Maana anasubiria mumchague tena

Ova
 
Maji yanaweza kweli yasitoke au yakawa hayatoki naunga mkono hoja kuusu usumbufu wa maji kuto kutoka toka iyo ipo kila baadhi ya maeneo lakini kwenye wiki mbili kutokutoka hapana tena nakataa mtoa post ivi unazijua vizuri week mbili kweli?
 
Wee unashangaa wiki mbili tena hao segerea washukuru huku Kinyerezi hasa kuanzia makofia kwenda mpk kifuru mnaweza kukaa hadi wiki nne+ plus hakuna maji inabidi muagize tu ya kwenye magari

Wao sasa ukiwa hujalipa bill sms kama mvua tunakusisitiza, bill hii ni notisi mimi huwa naziangalia tu nalipa napojisikia au nalipa kidogo tu
 
Maji yanaweza kweli yasitoke au yakawa hayatoki naunga mkono hoja kuusu usumbufu wa maji kuto kutoka toka iyo ipo kila baadhi ya maeneo lakini kwenye wiki mbili kutokutoka hapana tena nakataa mtoa post ivi unazijua vizuri week mbili kweli?
Unakataa una uhakika au unakataa, watu wamekaa week 2 hakuna maji, eti we unakataa.
 
Kukata maji bila tqarifa ni kunihujumu uchumi wangu binafsi.
 
Sisi huku Bunju tunamwagilia migomba , matango na matikiti maji kiroho safi kabisa...

Poleni sana wazee wa Ilala...
 
Back
Top Bottom