KERO DAWASA shughulikieni hii chemba ya maji taka inayomwaga maji ya kinyesi ILALA sokoni, Mtaa wa TABORA na UHURU mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Taarifa hii iende moja kwa moja kwa mamlaka ya Maji safi na maji taka mkoa wa Dar-es-salaam, DAWASA na wadau wote wa mazingira na Afya kwa ujumla.

Hali ya mtaa wa tabora na uhuru ni mbovu sana kutokana na chemba ya maji taka kuziba na kutiririsha maji taka yenye kinyesi barabarani ambapo wafanyabiashara wa soko la mbogamboga na matunda ILALA hupanga bidhaa zao.

Pia, soma; √ - DAWASA: Chemba ya maji taka iliyokuwa inamwaga maji ya taka Ilala sokoni, imetengenezwa

Tunatoa wito kwa mamlaka inayoshugjulikia maji safi na maji taka kutatua kero hii ambayo endapo haitadhibitiwa kww haraka basi kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka kwa magonjwa ya milipuko kama Kipindupjndu na homa ya matumbo.

Cha ajabu eneo hili lipo mkabala kabisa na zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam na mkuu wa wilaya ya Ilala. Mh Chalamila toka ofisini na wadau wako mje kuona kadhia hii na kutoa suluhisho la haraka kabla hali ya hatari haijatokea.

Wasalam.
 

Attachments

  • IMG_20241213_171252_613.jpg
    471.3 KB · Views: 4
Oya Chala umeona makimba yako yanaelea hapo au unajifanya hauoni?
 
Narudia tena mazingira sio salama kabisa kwa afya za raia.

Isijetokea shida baadae tuanze kusema ni mipango ya shetani juu ya Maza, watanzania tuingie kwenye mfungo wa siku kadhaa na maombi.

Mamlaka husika yadeal na shida za raia. Ni ngumu sana kumshawishi mtu hapo ni Dar.
 
Hali inatisha mno ukizingatia wapo watu wanauza na kula chakula maeneo hayo
 
Dar jiji la vinyesi kila sehemu mvua ikinyesha ndio utaelewa hasa hasa hayo maeneo ya hapo mjini watu wanakunya sana na sewage system ilivyo mbovu jamaa wanavizia mvua inyeshe waachie makimba kwenye mitaro, sehemu zote zenye guest lodge na hotel ndio balaa wanavizia mvua waachie makimba yaende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…