Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Taarifa hii iende moja kwa moja kwa mamlaka ya Maji safi na maji taka mkoa wa Dar-es-salaam, DAWASA na wadau wote wa mazingira na Afya kwa ujumla.
Hali ya mtaa wa tabora na uhuru ni mbovu sana kutokana na chemba ya maji taka kuziba na kutiririsha maji taka yenye kinyesi barabarani ambapo wafanyabiashara wa soko la mbogamboga na matunda ILALA hupanga bidhaa zao.
Pia, soma; √ - DAWASA: Chemba ya maji taka iliyokuwa inamwaga maji ya taka Ilala sokoni, imetengenezwa
Tunatoa wito kwa mamlaka inayoshugjulikia maji safi na maji taka kutatua kero hii ambayo endapo haitadhibitiwa kww haraka basi kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka kwa magonjwa ya milipuko kama Kipindupjndu na homa ya matumbo.
Cha ajabu eneo hili lipo mkabala kabisa na zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam na mkuu wa wilaya ya Ilala. Mh Chalamila toka ofisini na wadau wako mje kuona kadhia hii na kutoa suluhisho la haraka kabla hali ya hatari haijatokea.
Wasalam.