Dawasa tangu aondoke Eng. Luhemeja tunakoma

Dawasa tangu aondoke Eng. Luhemeja tunakoma

Sawa na Mbezi Makabe huku maji yalikuwa yanatoka kila siku ila toka dec mwaka jana wakaanza kuyakata wiki hii maji wameyaachia jumatatu tu mpaka leo kukavu na taarifa hakuna.

Bado maji kutoka machafu.
 
Huku Ukonga wanayaleta Ila ni tope hayafai hata kumwagilia sijajua shida Nini maji ya dimbwi Yana afadhali
 
Mboni huku Maji masafi mpaka tunajiuliza tupo Ulaya au tupo peponi, maji yananyweka kabisa bila shida huku nilipo Mimi maji ni masafi sana mpaka una tabasamu, kongole kwa Waziri wa Maji Juma Aweso anapiga kazi sana na DAWASA sio TANESCO,

Kwanza niliwahi kulalamika humu kuhusu hilo suala la water treatment sasa naona limefanyiwa kazi huku Maji yanakuja yananukia Dawa kabisa km yamewekwa water Guard unaoga maji km unaoga maji ya Uhai huku tena hatununui makatoni ya maji na kuishi na machupachupa kitu bombani na hatuumwi

TANESCO ndio wana tabia za kisengerema sio DAWASA
 
Huku Ukonga wanayaleta Ila ni tope hayafai hata kumwagilia sijajua shida Nini maji ya dimbwi Yana afadhali
Labda huko huku ni kitu mukide maji masafi sana, yamefanyiwa tiba ukiletewa maji machafu kipindupindu na homa za matumbo kinakua ndugu yako wa damu Baba mmoja Mama mmoja
 
DAWASA & TANESCO wanazingua sana.
Sio kweli DAWASA sio TANESCO usiwaringanishe kabisa huku hatukosi maji wiki nzima km yatakatika ni masaa tu yanatoka labda usipolipa ndio wanakukatia Ila km unalipa maji unamletea masafi
 
HAMENI
HAMNA MAKWENU..!

wazaramo wa watu wamebanwa tu na wahamiaji
 
Huu mlipuko wa kipindupindu nchini si ajabu ni matokeo ya hii kadhia ya kukosekana maji ya bomba watu wanatumia maji ya kwenye madimbwi huku wengine wakitapisha vyoo.
 
Hii mamlaka ya maji Dar na Pwani tangu aondoke Eng Luhemeja imekuwa kero tupu.

Mgawo wa maji kila mara pamoja na kwamba mvua zinanyesha kila siku wiki moja.

Sasa wakazi wa Kimara hatuna maji na bila hata taarifa kama kuna shida au mgawo.
Luhemeja kaachia ofisi?/Katenguliwa?
 
Hii mamlaka ya maji Dar na Pwani tangu aondoke Eng Luhemeja imekuwa kero tupu.

Mgawo wa maji kila mara pamoja na kwamba mvua zinanyesha kila siku wiki moja.

Sasa wakazi wa Kimara hatuna maji na bila hata taarifa kama kuna shida au mgawo.
Sisi wa majohe gongo la mboto tumetimiza mwezi na wiki mbili bila maji na hatujui sababu ni nn maana km mvua zinanyesha za kutosha
 
Kunywa bia kama maji shida
Walevi bwana,ulichoandika hapa wewe unakiona kinawezekana ktk maisha ya kawaida ya kila siku?

Sisi tunajadili jambo siriaz wewe unaleta pombe zako hapa?kuwa mstaarabu.
 
Back
Top Bottom