DAWASA: Ujenzi wa Bwawa la Kidunda (Morogoro) linalojengwa katika mkondo wa Mto Ruvu umefikia 27%

DAWASA: Ujenzi wa Bwawa la Kidunda (Morogoro) linalojengwa katika mkondo wa Mto Ruvu umefikia 27%

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imethibitisha kuwa ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro umefikia hatua ya Asilimia 27, huku mradi ukitarajiwa kukamilika ifikapo Mwaka 2026 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 336.

Imweelezwa kuwa bwawa hilo linajengwa kwenye mkondo wa Mto Ruvu na linatarajiwa kuhifadhi hadi Lita Bilioni 190 za maji.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Mkama Bwire amesema hiyo ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika, hasa wakati wa ukame katika maeneo yanayopata huduma kupitia mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Ameongeza kuwa mbali na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, mradi huu unatarajiwa kuchangia maendeleo ya viwanda, kilimo, na kuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla katika Bwawa la Kidunda.

Balile azungumzia Bwawa la Kidunda
Akizungumza kuhusu bwawa hilo, Mwanahabari mkongwe, Deodatus Balile ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) amesema:

“Kwa muda mrefu Vyombo vya Habari vimekuwa vikiandika kuhusu changamoto ya uhaba wa maji Jijini Dar es Salaam na vilieleza kuwa suluhisho la changomoto hiyo ni ujenzi wa Bwawa la Kidunda.

“Hili Bwawa lilifanyiwa utafiti wa kwanza Mwaka 1961 lakini halikujengwa, lilibaki kwenye maandishi, baada ya Vyombo vya Habari, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia ikaamua kuanza kulijenga.

“Mtendani (wa DAWASA) amesema bwawa hili litakapokamilika Juni 2026 linatarajiwa kutatua changamoto kubwa ya uhaba wa maji Dar es Salaam na amesisitiza inamaanisha suala la mgao wa maji itakuwa ni historia na Mto Ruvu hautakauka maji kwa kuwa bwawa hili litakuwa ni sehemu ya chanzo cha kuulisha mto huo.

“Tunavipongeza Vyombo vya Habari wa kuendelea kupaza sauti na kuripoti vila kuchoka kuhusu uhaba wa maji.

“Tunaamini miradi kama hii ambayo inatumua gharama kubwa itakuwa ni suluhisho la kupunguza changamoto ya uhaba wa maji maeneo mengi nchini.”

Snapinst.app_476095514_966108618952709_727592459549399350_n_1080.jpg
Snapinst.app_476250149_966108625619375_3570220414055354482_n_1080.jpg
Snapinst.app_476409693_966108632286041_6301220089346871047_n_1080.jpg

Meneja Sehemu ya Mazingira na Uratibu wa Jumuiya za Watumia Maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Janeth Kisoma ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Bodi ya Maji - Bonde la Wami Ruvu, ambao wapo chini wa Wizara ya Maji wakiwa na jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji chini ya Sheria za Rasilimali za Maji Namba 11 ya Mwaka 2009 na Marekebisho yake ya Mwaka 2022, ametoa neno.

Anasema “Majukumu yetu ni kufanya tathimini ya rasilimali za maji na kuhakikisha tunagawa rasilimali hizo kwa kuwa watumiaji wa vyanzo vya maji ni wengi, hivyo lazima kuwe na taratibu maalum za kusimamia kwa kuwa kuna kiasi cha maji ambacho kinatakiwa kubaki kwa matumizi mengine.

“Bodi tupo tayari kuusimamia na kuupokea mradi huu na kusimamia ili kuhakikisha kiasi cha maji hakipungui ndani ya bwawa, mnakumbuka hapo kati kulikuwa na changamoto ya maji kupungua kwa kiasi kikubwa katika Mto Ruvu? Hali hiyo ilichangia kuongeza uhaba wa wa maji.

Bwawa kuwa Pori Tengefu
“Tunafanya jitihada mbalimbali za kusimamia bwawa hili kwa kulitunza na kulitangaza kuwa eneo tengefu. Bwawa hili lina upana wa Mita 500 na Kilomita Square Mita 55, pia tunafanya jitihada za kuhakikisha linatangazwa kuwa bwawa tengefu katika Gazeti la Serikali.


==============================

Ikumbukwe hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima alisema utekelezaji wa mradi wa Bwawa la Kidunda utakapokamilika utaibua fursa nyingi za kimaendeleo ndani na nje ya Mkoa huo.

Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda unaogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 336 utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Juni 18, 2023 hadi Disemba, 2026, ukitekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na kusimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).

Jumanne ya Februari 4, 2025, Malima amefanya Kikao baina yake na DAWASA iliyoongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Mkama Bwire kwa lengo la kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi.

"Mradi huu ni muhimu sana kwakuwa utachochea fursa nyingi za maendeleo mkoani hapa, maendeleo ya miundombinu ya barabara toka Ngerengere hadi Kidunda umbali wa Km 75, Uzalishaji Umeme, Uboreshaji huduma ya Majisafi kwa vijiji vinavyopitiwa na Mradi, sambamba na kutoa ajira kwa wananchi wa Kidunda na maeneo jirani," amesema Mhe. Malima.

Kwa upande wake, Mhandisi Bwire ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 336 na kuridhia kuanza kwa utekelezaji wa mradi huu muhimu utakaoenda kuboresha upatikanaji huduma ya maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Miongoni mwa wadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Musa Kilakala, Taasisi za Bonde la Wami-Ruvu, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Morogoro.

Pia soma:
~
Wakazi wa Kimara na kata zake hawana maji zaidi ya wiki sasa, DAWASA hamuelezi maji yatatoka lini!
~ Ubungo riverside hatuna maji kwa siku 14 sasa
~ Uhaba wa maji mtaa wa Simba, kata ya Kilungule Bunju Beach
 
Hii miradi wanaichangamkia kipindi hiki kuelekea uchaguzi ili wapate cha kusema wakati wa kampeni, janjajanja sana hawa
🚮🚮

Mradi umeanza kujengwa mwaka juzi unaleta upuuzi wako saizi?

Samia ana maelfu ya miradi sio tuu ya kusema Bali ya kuonesha across sectors
 
Kwa mujibu wa mkataba, je ulianza lini na na unatarajia kuisha lini?
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza kuwa ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro, linalojengwa kwenye mkondo wa Mto Ruvu limefikia 27%, Pia linatarajiwa kukamilika 2026, likiwa na uwezo wa kutunza lita milioni 190 za maji.
Snapinst.app_476409693_966108632286041_6301220089346871047_n_1080.jpg

Snapinst.app_476250149_966108625619375_3570220414055354482_n_1080.jpg

Snapinst.app_476095514_966108618952709_727592459549399350_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom