Pre GE2025 DAWASA: Usambazaji wa maji Kinondoni wafikia 97%, Je, ulipo bado kuna shida ya maji?

Pre GE2025 DAWASA: Usambazaji wa maji Kinondoni wafikia 97%, Je, ulipo bado kuna shida ya maji?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA) @dawasatz Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni kufikia asilimia 97%.

Akizungumza katika Kikao Kazi cha DAWASA na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya ya Kinondoni, Mhandisi Bwire amesema “Tuchukue nafasi hii kumshukuru Mheshimwa Rais kwa kinondoni kazi ya maji imefanyika na bado kazi inaendelea kufanyika”

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa asilimia hizo 97% ni zile ambazo serikali imefikisha mtandao wa mabomba ikiwa inaendelea na kazi ya kuwavutia wateja wao maji.

“Kinondoni ina kata 20 mitaa 126 tumefika kwenye mitaa yote lakini kazi inaendelea. Serikali imefanya kazi yake ya kupeleka mtandao wa mabomba kwa 97% kuna kazi ya pili ya kuhakikisha ambapo sasa mtandao umefika watu wanajiunganisha kwenye mtandao huo”

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Wenyeviti wa mitaa ili kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma ya maji safi na salama.

Chanzo: Jambo TV
 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam(DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kinondoni kufikia asilimia 97%.
IMG-20250218-WA0039.jpg

Akizungumza katika Kikao Kazi cha DAWASA na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Wilaya ya Kinondoni, Mhandisi Bwire amesema “Tuchukue nafasi hii kumshukuru Mheshimwa Rais kwa kinondoni kazi ya maji imefanyika na bado kazi inaendelea kufanyika”

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mpaka sasa usambazaji wa maji kwa jiji la Dar Es Salaam umefikia asilimia 93% huku kwa Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni asilimia 97%.

“Kinondoni ina kata 20 mitaa 126 tumefika kwenye mitaa yote lakini kazi inaendelea. Serikali imefanya kazi yake ya kupeleka mtandao wa mabomba kwa 97% kuna kazi ya pili ya kuhakikisha ambapo sasa mtandao umefika watu wanajiunganisha kwenye mtandao huo” amesema Mhandisi Bwire.

Mhandisi Bwire ameeleza kuwa mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Wenyeviti wa mitaa ili kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na huduma ya maji safi na salama.
IMG-20250218-WA0039.jpg
IMG-20250218-WA0046.jpg
IMG-20250218-WA0047.jpg

IMG-20250218-WA0049.jpg
 
Back
Top Bottom