DAWASA, WADAU WAKUTANA KUJADILI MABORESHO MKATABA HUDUMA KWA WATEJA

DAWASA, WADAU WAKUTANA KUJADILI MABORESHO MKATABA HUDUMA KWA WATEJA

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
201
Reaction score
121
WhatsApp Image 2026-08-20 at 20.46.21 (2).jpeg

Wadau wa huduma za maji katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani wamekutana kujadili na kutoa maoni kuhusu maboresho ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), hatua inayolenga kuongeza uwazi, uelewa na ubora wa huduma kwa wananchi.

Katika kikao hicho, DAWASA imeeleza kuwa uboreshaji wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja hufanyika kila baada ya miaka mitano na hutoa nafasi kwa Wananchi, Wateja na watumiaji wa huduna za Maji kutoa maoni na ushauri juu ya maboresho hayo.

Mabadiliko yaliyofanyika katika Mkataba wa huduma kwa Wateja ni pamoja na urahisi wa Mawasiliano kutoka namba ya zamani ya huduma kwa wateja 0800110064 namba 181, uwepo wa mfumo wa kuomba huduma za miunganisho ya huduma za Maji kimtandao.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 20.46.21 (1).jpeg

Aidha, maboresho mengine ni kuondoa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) katika huduma za Usafi wa Mazingira hatua inayolenga kupunguza gharama kwa Wananchi wanaotumia huduma hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Lydia Ndibalema, amesema maboresho hayo ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka kuhakikisha wateja wanapata huduma bora, kwa haraka na kwa uhakika.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 20.46.21.jpeg

Amesema ushirikishwaji wa wadau ni muhimu katika kuboresha huduma kwa kuwa maoni yao yanaisaidia DAWASA kubaini changamoto zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi kwa wakati.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Ilala, Seif Mwela, ameipongeza DAWASA kwa maboresho yaliyofanyika na ushirikiano unaoendelea kati ya Mamlaka, viongozi na wananchi. Amesema huduma bora na ya uhakika inahitaji ushirikiano wa pamoja pamoja na wananchi kutimiza wajibu wao wa kulipia huduma.
WhatsApp Image 2026-08-20 at 20.46.22.jpeg
 
Back
Top Bottom