Dawasa wanatupiga

Dawasa wanatupiga

mayome

Member
Joined
Jan 17, 2012
Posts
62
Reaction score
21
Nimefanya tathimini nikagundua hizi mita za maji hapa Dar ni majanga sana. Yaani hata ukiwa umesafiri bili inakuja ileile na mita inatembea.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye mita za maji jamaa wanatupiga. Wanatuumiza sana jamani was galleries tena ufanisi wa mita zao.
 
Mimi hawa siku hizi sina shida nao. Nilikuwa nina mita kila mwezi bill inakuja 60, 50 nikawalalamikia wakaja wakaibadili fasta wakaweka mpya, toka siku hiyo bill ilidrop ni 20, 18, 14.
Hata nikiwa na tatizo nikipga simu wakasema wanakuja wanakuja kweli
 
Hawa DAWASA hapana kabisa kwani hata mimi siwaelewi kabisaa.Kwani kwangu mita haionyeshi kabisa namba lakini wao wakija wanasoma na kuondoka,nishamweleza tatizo msoma mita lakini wapi,panapo majaliwa nitawakimbia tu
 
Lipeni TOZO acheni makasiriko kwanza mlishaambiwa kama mkiona vipi hamieni Burundi tu maana hakuna namna sasa.
 
Nimefanya tathimini nikagundua hizi mita za maji hapa Dar ni majanga sana. Yaani hata ukiwa umesafiri bili inakuja ileile na mita inatembea.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye mita za maji jamaa wanatupiga. Wanatuumiza sana jamani was galleries tena ufanisi wa mita zao.
Meter za Dawasa ziko vizuri,Funga gate valve unaposafiri!
Miundo mbinu ya Ndani huwa ni Changamoto kwa wengi,na mlio wengi hamuikagui mnabaki kuwalaumu dawasa
 
Wanachofanya wao wanapita kwenye ile average bill yako wanakua wana ongeza na kupunguza kidogo
 
1. Kiuhalisia ukiona mabadiliko ya bili, chunguza huenda kuna mahali maji yanavuja (leakage)
2. Gharama ya unit naona wameongeza bei kidogo
Yes
Leakage kwenye Miundo mbinu hasahasa ya ndani
 
1. Kiuhalisia ukiona mabadiliko ya bili, chunguza huenda kuna mahali maji yanavuja (leakage)
2. Gharama ya unit naona wameongeza bei kidogo
Hamna cha leakage wala nini, nyumbani kwetu tulitafuta hiyo leakage hadi basi
Halafu leakage hata kama ingekuwa kubwa kiasi hicho,

Mfano kuna kipindi tumepima maji kabisa tuliyotmia kwa mwezi kwenye simtank

Tulitumia simtank 4 za ujazo wa lita 2000 ambazo ni lita 8000 sawa na unit 8, ila matumizi bili ikaja unit 37, na mita zinasoma tumetumia unit hizo kweli
Sasa unit 8 hadi 37, leakage kubwa kiasi hicho ingeonekana tu
 
Leakage gani tena. Na maji tunajaza kwenye Tank yanafungwa bombani

Na tank inajulikana ina ujazo gani na inatumika siku ngapi

Kwa mwezi inajulikana wazi zimetumika tank kadhaa

Watuambie tu unit moja siyo ndoo 50
 
Waziri Aweso pmoja na watendaji wa DAWASA Mkoa wa DSM tafadhali sikilizeni na fuatilieni kilio cha wananchi wa Mkoa wa DSM juu ya malalamiko yao ya mita kutokosomeka.

Tatueni hiii changamoto maana malamiko ni mengi sana kuhusu Usomaji wa mita, either mita ni mbovu au tatizo ni wasoma mita?
 
Inawezekana meter ni mbobu kweli.

Ila kwa upande wangu iko hivi.....

Huwa naweka kumbukumbu za matumizi ya kila mwezi (unit).

Kwa mfano ..matumizi ya maji September ni unit 59.

Yaani last time meter ilisoma 1813, na hadi juzi walikuja kusoma meter na kukuta 1872.
Hapo unachukua Current reading - previous reading ( 1872-1813) = 59 Unit.
Huwa nathibitisha kama alichosoma mosoma mita ni sahihi.

Then najiandaa kulipa bill, na hapo nakaa nikijua pesa nitakayolipa.

Unit moja ni 1,680/=

Data zangu na data za Dawasa hazijawahi kukinzana.
 
Back
Top Bottom