Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hususani eneo la Ilala na Kariakoo, kwa lengo la kuhakikisha mifumo ya majitaka inafanya kazi kwa ufanisi na mazingira yanakuwa salama na rafiki kwa wananchi. Zoezi hilo linahusisha kusafisha na kuimarisha mtandao wa majitaka pamoja na kufanya matengenezo ya chemba za majitaka zilizopo katika maeneo hayo.
Katika utekelezaji wa zoezi hilo, DAWASA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha miundombinu ya majitaka inakuwa katika hali nzuri ili kuzuia majitaka kutiririka mtaani na kuathiri mazingira ya wananchi, uboreshaji huu Ukiwa sehemu ya juhudi za Mamlaka kuhakikisha huduma za usafi wa mazingira zinapatikana kwa ufanisi, hususan katika maeneo yenye shughuli nyingi za biashara na makazi kama Ilala na Kariakoo.

Sambamba na kazi hizo, DAWASA imewasihi wananchi kuwa sehemu muhimu ya kulinda na kutunza miundombinu ya majitaka kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mifumo hiyo na kuepuka tabia ya kujiunganisha kiholela katika mifumo ya majitaka, wananchi wamekumbushwa kuacha tabia ya kutupa taka ngumu kwenye mifumo hiyo, kwani taka hizo zinaweza kusababisha kuziba kwa mabomba na chemba, hivyo kusababisha majitaka kujaa na kuathiri mazingira.
Niwaombe wananchi wote uedelea kutoa taarifa mapema kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 181 wanapoona uharibifu au hujuma dhidi ya miundombinu ya majitaka ili miundombinu hii iweze kutumika kwa muda mrefu kwa manufaa ya jamii nzima" ameeleza Mhandisi Mubaraka Mpala kutoka idara ya Usafi wa Mazingira.
DAWASA inaendelea kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya Mamlaka na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya Jiji yanakuwa safi na salama. Uboreshaji na utunzaji wa mifumo ya majitaka unasaidia kupunguza hatari ya milipuko ya magonjwa yanayotokana na uchafuzi wa mazingira, ikiwemo kipindupindu, pamoja na kuboresha afya na ustawi wa jamii kwa ujumla.