DAWASA yafafanua sababu za Wakazi wa Muheza Kibaha kukosa huduma ya maji kwa wiki nzima

DAWASA yafafanua sababu za Wakazi wa Muheza Kibaha kukosa huduma ya maji kwa wiki nzima

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya malalamiko ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai Wananchi wa Mtaa wa Muheza na Tankini, Kibaha-Maili Moja Mkoani Pwani hawana huduma ya maji kwa muda wa wiki moja, Mamlaka imeto ufafanuzi.

Kusoma malalamiko ya Mdau, bofya hapa ~ Wananchi wa Tankini na Muheza - Kibaha hatuna huduma ya maji wiki sasa, DAWASA hawatupi majibu ya kueleweka

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Everlasting Lyaro amesema:

Hili eneo la Muheza kuna Mkandarasi wa TARURA alipitisha greda kwa ajili ya kutengeneza Barabara kuanzia siku ya Jumatatu mpaka Jumanne ya week iliyopita.

Akakata mabomba ya nchi 6 ambayo yanasambaza huduma ya maji eneo la Maili Moja mpaka Mpiji.

Juzi tumelitengeneza baada ya Mkandarasi kununua vifaa vinavyohitajika.

Kazi imefanyika juzi na kukamilika.
photo_2024-07-21_13-46-41.jpg

photo_2024-07-21_13-46-40.jpg

photo_2024-07-21_13-46-37.jpg
 
Dodoma Kikuyu Extension wameweka njia za vivuko kimmoja kwa watembea kwa miguu ambacho ni kimmoja kikuyu SGR imekuwa ni mateso kwa watu wa Hali ya chini pia kwa wanafunzi ambacho asubuhi itabidi wazunguke umbali mrefu kukifata kivuko ili wasivuke kitu ambacho kinasumbua sana tunaomba uongozi wa TRC waweke kivuko cha watembea kwa miguu kama ilivyo mbezi magufuri stand kipite juu ili kuweza kukidhi naitaji ya mitaa yetu maana tumechoka kuzunguka umbali ule kwakweli
 
Back
Top Bottom