DAWASA yaja na operesheni siku 90 kudhibiti upotevu wa maji

DAWASA yaja na operesheni siku 90 kudhibiti upotevu wa maji

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Bwire atangaza vita mpya dhidi ya upotevu wa maji Dar na Pwani

DAWASA yalenga kushusha upotevu wa maji hadi asilimia 20

DAWASA yaomba ‘tafu’ kwa Wananchi kubaini upotevu wa maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetenga siku 90 za kutekeleza mpango maalum wa kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma ya majisafi na kuongeza ufanisi wa miundombinu yake.

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa kudhibiti upotevu wa maji, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema Mamlaka imejiwekea siku 90 za kupambana na upotevu wa Maji na hatua za awali zimeanza kwa ukarabati na ubadilishaji wa miundombinu chakavu inayochangia mivujo na upotevu mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ya kihuduma.

“Kama mnavyofahamu, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) alitoa taarifa kuwa kiwango cha upotevu wa maji katika Mamlaka nyingi nchini kimefikia asilimia 35. Kutokana na hali hiyo, DAWASA tumeanza kuchukua hatua mahsusi kwa kutenga siku 90 za kushughulikia changamoto hii,” amesema Mhandisi Bwire.

Ameeleza kuwa mafanikio ya mpango huo yatategemea ushirikiano wa karibu kati ya DAWASA na wananchi, huku Mamlaka ikiahidi kutoa zawadi kwa watu watakaosaidia kutoa taarifa za mivujo ya maji na maeneo yenye upotevu mkubwa wa huduma hiyo.

“Katika utekelezaji wa mpango huu tutashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo watumiaji na wasiokuwa watumiaji wa huduma ya maji, pamoja na makundi maalum kama mama lishe, maafisa usafirishaji (Bodaboda), viongozi wa serikali na jamii kwa ujumla,” ameongeza.

DAWASA imebainisha kuwa lengo lake ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kiwango cha upotevu wa maji kinashuka hadi kufikia asilimia 20, kiwango kinachokubalika kimataifa katika sekta ya maji.

Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya muda mrefu ya Mamlaka katika kuboresha usimamizi wa maji, kuongeza mapato, kulinda rasilimali ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika kwa ufanisi zaidi.
IMG-20260518-WA0015.jpg
IMG-20260518-WA0016.jpg
IMG-20260518-WA0014.jpg
IMG-20260518-WA0010.jpg
IMG-20260518-WA0007.jpg
IMG-20260518-WA0004.jpg
IMG-20260518-WA0004(1).jpg
 
Waje banana ukonga karibu na aviation house maji yanatiririka kama mfereji wa humuzi
 
Huyu Bwire ndio aliambiwaga:
“Engineer soma hukoooooo..”
Alivokuaga Tabora.
 
Huyu Bwire ndio aliambiwaga:
“Engineer soma hukoooooo..”
Alivokuaga Tabora.
Ndiyo.. Huyu Injia Aweso alimtoa huko tabora akamleta Dar. Janja janja Dawasa imepungua sana.
 
Ndiyo.. Huyu Injia Aweso alimtoa huko tabora akamleta Dar. Janja janja Dawasa imepungua sana.
Hapo sawa. Atatue sasa changamoto ya Kigamboni na Mbagala ambayo wenzie wote wameishindwa.
 
Wajenzi wa barabara wanaharibu sana miundombinu ya maji ,kuna jamaa alileta greda akapasua bomba kubwa la nchi 6 ,siku narudi nakuta bwawa la maji.


Dawasa watoe pesa kwa watu wanaolipoti upotevu wa maji na watu wanaoharibu miundombinu ya dawasa walipe gharama za marekebisho.
 
Back
Top Bottom