DAWASA yakanusha taarifa za upungufu wa Maji Mto Ruvu

DAWASA yakanusha taarifa za upungufu wa Maji Mto Ruvu

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, amesema kuwa hali ya maji katika Mto Ruvu ni ya kutosha, hivyo wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wasiwe na hofu ya upungufu wa maji.

Mhandisi Bwire ameyasema hayo leo, Machi 11, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhandisi Bwire amesema kuwa hivi karibuni baadhi ya watu ambao si wapenda maendeleo ya DAWASA walisambaza video kwenye mitandao ya kijamii wakidai kuwa maji yamepungua kwenye Mto Ruvu. Hata hivyo, ameeleza kuwa video hiyo ni ya muda mrefu na si ya sasa, hivyo amewahakikishia wakazi wa mkoa huo kuwa maji yapo ya kutosha.

Aidha, Mhandisi Bwire amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kuna zaidi ya mita 16.7 ya maji katika mto huo wa Ruvu na mvua zinazotarajiwa kunyesha zitasaidia kuongeza maji katika bwawa hilo.

 
Back
Top Bottom