Hapa nilipo leo ni wiki ya pili hakuna Maji.
Kuna wengine hapa hapa Dar na Pwani wanalalamika kuwa ni zaidi ya mwezi hakuna Maji. Arusha, Morogoro na miji mingine kama Dodoma hali ni hiyo hiyo.
Matukio kama haya ndiyo yanayopaswa kuwakumbusha Watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwa siku zote Wanapaswa kusimamia Haki pamoja na misingi ya Utawala Bora maana wakisimamia hayo Wananchi watapata viongozi sahihi wenye akili, uwezo na majibu sahihi na ya kudumu ya changamoto zinazowakabili.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama badala ha kuwalinda Wananchi na Maslahi yao, wanalinda kikundi kidogo cha Watu kinacholazimisha kuwatawala Wananchi bila ridhaa yao, tena kwa nguvu na hata kuwaua, kuwabaka, kuwapoteza, kuwafungulia kesi za uongo na kuwalawiti.
Matokeo yake ndo haya. Viongozi wanaolazimisha kuwatawala Wananchi hawaoni haja ya kuwajibika kweli kwa Wananchi. Hawaoni haja ya kutafuta suluhisho la kudumu juu ya Matatizo yanayowakabili wananchi maana wana uhakika wa kuiba chaguzi na kuwalazimisha wananchi kukubali chochote kwa mtutu wa bunduki. Wao wanachoangalia ni kujinufaisha binafsi na familia zao.
Katika karne hii ya 21, wakati wenzetu wakifikiria kwenda kuishi sayari nyingine, na Mataifa mengine ambayo yapo Jangwani kama Israel hawana mgao wa Maji, hapa Tanganyika Samia, familia yake, ndugu zake na chama chake wanawaibia wananchi, wanalazimisha kuwatawala kwa nguvu huku Wananchi wakipata shida ya mgao wa Maji.
Cha ajabu zaidi Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinatumika kumlinda huyu mtu Samia na genge lake ili azidi kufanikisha mateso ya Watanganyika.
View attachment 3512138