DAWASCO ina aina tofauti za mita au mita zote zinafanana kwa matumizi?

DAWASCO ina aina tofauti za mita au mita zote zinafanana kwa matumizi?

kaka kikatiba

Member
Joined
Oct 15, 2014
Posts
8
Reaction score
4
Nimekua nikipata tatizo la bili ya maji kuongezeka sana kias kwamba ninapata waswas maana tangu nibadilishiwe mita iliyokuwa imefubaa haisomeki vzuri, sahiz bili ya maji inakuja kubwa mpaka natamani irudishwe ya awali.

Kama kuna mtu ana uelewa anijuze hizi mita zina utofauti upi isijekuwa nimefungiwa ya matumizi ya kiwanda!
 
Na Mimi nasubiri majibu. Meter zao za siku hizi nimezishtukizia. Ngoja wataalam waje kujibu.
 
Mita inasoma units (kiasi gani umetumia yaani lita kadhaa) charges wanazikokotoa baada ya kupata hizo units kwahio kama wewe upo tariff ya matumizi ya juu ni katika calculation baada ya kupata units, cha maana soma units mwenyewe alafu cheki nao kama upo tariff ya biashara.

Pia jaribu kufunga maji nyumba nzima alafu cheki kama mita inazunguka sometime kuna leakage sehemu hivyo kupelekea maji kutumika kwa wingi
 
Mita nzuri ji zile za chuma, hizi za plastic ni kimeo hatari.

Hata upepo kwenye Bomba ukipita inazunguka kwa kasi na kuongeza units
 
Ukiona una mashaka na mita yako, unawasiliana na DAWASA wanaichukua for calibration BUREE.
 
Nimekua nikipata tatizo la bili ya maji kuongezeka sana kias kwamba ninapata waswas maana tangu nibadilishiwe mita iliyokua imefubaa haisomeki vzur,sahiz bili ya maji inakuja kubwa mpaka natamani irudishwe ya awali!
Kama kuna mtu ana uelewa anijuze hizi mita zina utofauti upi isije kuwa nimefungiwa ya matumiz ya kiwanda!
Hapo kuna mawili ama matatu kwa uzoefu wangu:

Aidha hiyo mita iliyofubaa ilikuwa haisomwi vizuri na baada ya kuingo'a wameenda kugundua kwamba ilikuwa inakula kwao, sasa fidia wanakukata kidogokidogo.

Ama kuna mabomba uliyopitisha underground kwenye utandikaji yana leakage.

Hii sababu ya pili inatesa wengi.

kuna maeneo bomba lililochimbiwa likipasuka kwa chini, aridhi hufyonza maji hata bila kuonesha alama ya uharibifu, tumia mafundi kufuatilia.

Sababu ya tatu, kama ulikuwa unatumia unit kidogo(nimesahau kutoka sifuri hadi ngapi) bei huwa ni ndogo, ukizidi hapo wanadouble kama ilivyo kwenye umeme, maji hawana bei za flat rate kwenye malipo ya unit zao.

Kwa maelezo yako hayo wasiliana na mamlaka utapata ushauri pakuanzia na nini cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingine usifanye mazoea na msoma mita huwa wanatabia ya kubambika bili Ili uwaombe wakupunguzie, hakikisha na wewe unakuwa na record ya unit Ili ulinganishe.
 
Nimekua nikipata tatizo la bili ya maji kuongezeka sana kias kwamba ninapata waswas maana tangu nibadilishiwe mita iliyokua imefubaa haisomeki vzur,sahiz bili ya maji inakuja kubwa mpaka natamani irudishwe ya awali!
Kama kuna mtu ana uelewa anijuze hizi mita zina utofauti upi isije kuwa nimefungiwa ya matumiz ya kiwanda!
Wewe lipa bill bana
 
Soma units na mtu wa dawasco pamoja, weka kumbukumbu...

Ngoja waje kukupa muongozo...
 
Hata kwangu tangu wabadilishe mita ankara inayukuja sasa ni karibu mara dufu ya wastani wa awali, na ukilalamika wanakuta maelezo ya mkato mkato!
Nadhani wametufungia mita mbofumbofu ambazo zinatembea hata ikipulizwa na upepo tu!
 
Back
Top Bottom