BashiriOnline
Senior Member
- Nov 5, 2012
- 127
- 44
Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai
kuwa msanii wa zamani wa kundi Daz Nundaz
na hitmaker wa Figure Namba 8′ Daz Baba
amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni
kuonekana akifanya vitendo ambavyo havilingani
na mtu mwenye akili timamu.
Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo
ya Morogoro akiwa katika hali iliyowatia mashaka
ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii
wenzake.
Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia
mwandishi wetu jana akiwa mkoani Morogoro
kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili
zote za mtu ambaye ni Kichaa na amekuwa
mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya
matukio ya ajabu.
Hivi juzi juzi Daz alienda nyumbani kwa Afande
usiku, akapiga kelele sana, Afande akaamka na
kumkuta Daz akiwa mchafu na akiongea maneno
ambayo hayaeleweki, baadaye alitaka kumfanyia
tendo baya kwa mfanyakazi wa kike wa Afande
lakini hakufanikiwa, ila watu wakajua kweli Daz
hayuko sawa, alisema.
Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu alimtafuta
Afande Sele, ndipo alipothibitisha kutokea kwa
tukio hilo nakusema ameshampatia taarifa dada
yake Daz wa Dar es salaam.
Kweli hali ya Daz ni mbaya sana nimejaribu
kumuweka sawa lakini nimeshindwa labda
wakamfanyie matambiko ya kwao kwasababu
baba na mama yake walifariki na walikuwa
hawaelewani labda kuna matatizo ya kifamilia.
alisema Afande.