DC Babati: Uvamizi maeneo ya serikali, Sitaki kumkuta mtu kwenye eneo la Serikali

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, ameonya vikali wale wote waliovamia maeneo ya wananchi na yale ya Serikali katika Kata ya Mamire, akiwataka kuyarejesha mara moja kabla hajachukua hatua kali.

Kaganda ameweka wazi kuwa Serikali haitavumilia vitendo vya uporaji wa ardhi, hasa maeneo ya malisho na yale yaliyo pembezoni mwa hifadhi za taifa, akisisitiza kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa wote watakaokaidi agizo hilo.

Maelekezo hayo yametolewa Machi 03, 2025, katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Mamire, ambapo mwananchi Asa Daniel aliwasilisha malalamiko kuhusu uvamizi mkubwa wa maeneo ya malisho katika eneo la Baraguu na maeneo mengine.

Asa alieleza kuwa robo tatu ya ardhi ya malisho imevamiwa, hali inayowaletea changamoto kubwa wafugaji wa eneo hilo.

Kaganda, akijibu hoja hiyo, amewataka wavamizi wote kuondoka mara moja na kurejesha maeneo hayo kwa matumizi yake sahihi kabla hatua kali hazijachukuliwa.

Amesema kuwa hakuna atakayeonewa huruma katika suala hili na kuwa Serikali ipo imara kulinda ardhi ya wananchi na mali za umma. Aidha, ameliagiza jeshi la polisi na viongozi wa kata kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanarejeshwa haraka kwa matumizi halali.

"Hapa Babati kuna DC, hapa Babati kuna Serikali. Sitaki kumkuta mtu kwenye eneo la Serikali, na wanaoota ota wafute kwa sababu Serikali ina mpango mzuri na nyie," alisisitiza Kaganda huku akiwatahadharisha wale wanaojaribu kutengeneza makundi ya ujanja ili kuvamia maeneo yasiyostahili.

Akihitimisha, Kaganda amewataka wananchi wa Mamire na Babati kwa ujumla kushirikiana na Serikali katika kulinda ardhi na rasilimali zao.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…