The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa wilaya ya Hai, Hassan Bomboko ameagiza kuondolewa kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Mabweni, Vyoo na Nyumba ya mwalimu katika shule ya Sekondari Saashisha kwa kile kinachotajwa kushindwa kutekeleza mradi huo unaotajwa kufikia asilimia 75.
Mradi huo wenye thamani ya kiasi cha sh Milioni 479 ulipaswa kukabidhiwa January 7 mwaka huu hata hivyo hadi sasa imeelezwa kuwa utekelezaji wake umekua wa kusuasua ikiwemo uwepo wa mafundi wachache ikilinganishwa na ukubwa wa mradi huo.