Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amesema kuwa hali ya usalama ni shwari katika vituo vyote vilivyopo katika vijiji 107 na vitongoji 813 katika Wilaya Hiyo ya Chamwino
Mhe. Mayanja ameyasema hayo Leo Nov 27,2024 wakati akizungumza na Wasafi Media kwenye kituo Cha kupiga kura Cha Sokoine Wilayani humo
Mhe. Mayanja amesema kuwa wamejipanga vizuri na ndio maana vituo vyote vina utulivu na amani na zoezi Hilo linaenda vizuri