DC Chauchau apewe nafasi ya kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam

DC! Naye ameridhia zile Baarbara za hovyo kabisa kuwahi kutokea Tanzania!? Au zimejengwa kabla yake!?

Zile barabara sijawahi ona popote tangu nimeanza kutembelea hii nchi!

Barabara ya Kigoma-Mwandiga via gungu!

Engineer alikuwa anawaza nini mpaka ku design Barbara ya aina ile na mkoa kuridhia ujenzi wake??

DC, Barabara zenu zimewafelisha sana viongozi wa Kigoma.
 
Kwaiyo saizi amekuwa dc! huyu jamaa sijuwi ni mtu wa kitengo! maana serikali inamuweka popote pale mfano kule kwetu aliwahi kuwa mbunge 2015-2020.
 
Chalamila bado sana , mtoe kwenye list
 
hizo kazikuta mkuu
 
Hogera bwana chuachua
 
chawa wa mpindimbi huwezi mlinganisha na chawa wa masaki ingawa wote ni wale wale.
 
Kazi ya kiongozi siyo ''kuzungumza kwa sauti ya mamlaka'' wana ''kutatua migogoro''. Haya mambo ya kudhani kazi ya kiongozi ni kutatua migogoro ndiyo yanafanya viongozi wetu waache kuongoza ili kuzuia matatizo na migogoro na badala yake wanafanya starehe huku wakisubiri migogoro na matatizo yatokee, wayatatue. Kuna vyombo maalum vya kutatua migogoro. Na zaidi, mfumo wa uongozi tulionao ndiyo tatizo, hivyo tushughulikie kiini cha tatizo.
 
kuzungumza kwa sauti ya mamlaka ni muhimu sana unapokuw kiongozi, ukiona huna sauti ya mamlaka ujue hata familia yako hutaweza kuiongoza. "ability to command".

sio kudhani kazi ya kiongozi ni kutatua migogoro, hapana ! kwa unyeti wa nafasi aliyonayo kama mwenyekiti wa baraza la usalama la wilaya, anayo haki ya kuintervene ili kuepusha possible escalations.

After all nikitumia ubishi wangu kukujibu ni hivi, kazi ya Ofisi za hao watu (umma) ni kutoa huduma kwa jamii, tafsiri ya kutoa huduma ni kutatua changamoto zinazowakumba wanajamii ikiwa ni pamoja na kila kitu kwenye maisha yao.

serikali ipo kukutatulia changamoto zako kama mwanajamiii, na kukuhakikishia uwepesi wa maisha !, hivyo ofisi hizo ziko centered hapo.
 
Ubongo wako umejaa kutu ya ki-bongobongo. Najua kwa mtu aliyezaliwa na kukulia Tanzania ni ngumu sana kuelewa ninachosema. Kiongozi anatakiwa awe na uwezo wa kushawishi na siyo kuamrisha (sauti ya mamlaka). Ni mara chache sana kiongozi atatumia sauti ya mamlaka! Pengine elimu yetu na kupigwa sana shuleni kumetengeza vichwa vyetu vidhani kuwa kutoa amri ndiyo kuongoza. Ndiyo maana ukisikiliza hotuba za viongozi wetu zimejaa amri za makatazo na vitisho na siyo ushawishi na kuelimisha. Kuhusu kutatua changamoto: Kazi ya kiongozi ni kuongoza ili kuzuia matatizo kwa jamii. Lakini kwa sababu kiuhasilia huwezi kuzuia matatizo yote, basi kiongozi mzuri ni yule anayeunda mechanism za kutatua hayo matatizo. Kuna mahakama, kuna polisi, kuna idaza za maji, kuna idara za kuzoa taka, zote hizi zinatakiwa kutimiza wajibu wake. Kama hazitimizi basi ni jukumu la kiongozi kuona zinatimiza kwa kuondoa wale viongozi wabovu. Mkuu wa mkoa ukiamua kutatua matatizo ya wananchi hutaweza kwa sababu yapo mengi na mkoa una watu wengi
 
unaweza kuwa na hoja lakini haifit kweny hili andiko.....unafahamu nafasi ya mkuu wa wilaya mbali na kuwa kiongozi pia ni mtawala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…