DC Chikoka ashiriki katika kukabidhi madawati 250 kwa shule za Wilaya ya Rorya

DC Chikoka ashiriki katika kukabidhi madawati 250 kwa shule za Wilaya ya Rorya

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
107
Reaction score
97
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka ameshiriki kukabidhi madawati 50 kati ya Madawati 250 ambayo yametolewa na Bank ya NMB kwa shule 5 zilizopo wilayani hupo kwa lengo la kusaidia kupunguza changamoto ya watoto kukaa chini na kuboresha ufaulu wao.

FuFCiVYXsAMQLVa.jpg


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, DC Chikoka amesema: "Tuwashukuru NMB sisi watu wa Rorya kutuwezesha kufikia lengo letu la mapambano ya kukabiliana na ufaulu mbovu, niwaombe walimu na Wanafunzi kutumia misaaada hii kama chachu ya kuongeza ufaulu wenu."

FuFBcGkWwAAV4pP.jpg


FuFCOAoXoAAOdYW.jpg

Naye, Meneja NMB Kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus amesema wamekabidhi madawati 250 yenye thamani ya Shilingi Milioni 24.9 kwa shule tano za Kengwa, Tacho, Nyamusi, Ngasaro, Nyihara zilizopo Wilayani Rorya, kusaidia Serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya Elimu na kurudisha kwa jamii.
 
Back
Top Bottom