Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe, amewapigia magoti Wananchi wa Vijiji vya Msikiii na Munkhola katika Wilaya hiyo ikiwa ni msisitizo wa kuwaomba waondoke katika eneo walilovamia la hifadhi ya Msitu wa Munkhola ambalo limeanza kupata mmomonyoko wa ardhi unaoweza kusababisha madhara kama yaliyotokea Hanang, Manyara.
Hatua hii imekuja baada ya Wananchi wa Kijiji cha Msikii na Munkhola kuvamia eneo hilo na kujimilikisha kinyume na utaratibu wa sheria na kufanya shuhuli zao na kusababisha mmomonyoko wa ardhi katika kijiji cha Munkhola ambapo nyumba zaidi ya 150 zimeharibika kutokana na chemchem inayotoka katika hifadhi hiyo.
Aidha, DC Gondwe ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Singida ndani ya siku 14iwe imetoa nakala kwa Wavamizi kuondoka katika eneo hilo na atakayekaidi agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao "kuharibu hifadhi ni ubinafsi, mvua mtapata wapi? hapo chini kijiji kitakwisha, yalitokea Hanang ndio hayo mnataka yatokee hapa achenii"