Mkt wa Kamati ya Usalama anapigia magoti wananchi mbele ya KU yake nadhani si sawa. Jambo walilofanya wananchi linahatarisha usalama wa watu hivyo ni hatua za haraka kuchukuliwa yeye ni mkt wa KU na ana vyombo vya kutosha. Kuna mbinu nyingi za kutumia kufanikisha hicho anachopigia magoti. Ameiga ya viongozi wa kisiasa kupiga magoti akina Jenista Mhagama. Wale ni political figures wanatafuta umaarufu na wanaomba zaidi kwa ajili ya wananchi wao. Yeye ni mtawala na msimamizi wa serikali Wilayani, ni maoni yangu kuwa hajawaza vyema kwenye hili.