kimarabucha
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 791
- 621
Wadau nimeshangazwa na kitendo cha Mkuu Wa Wilaya ya Handeni Bw.Gondwe kumchongea Hakimu aliyehukumu kesi ya mfugaji vs mkulima Kwa Mh.Rais kuwa eti Hakimu anawapendelea wafugaji.Matokeo yake Hakimu huyo amehamishwa.Nilitegemea Mkuu Wa wilaya ni Mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Sheria anazijua.Mahakama ikitoa HUKUMU kama hujaridhika ni kukata RUFAA tu sio KUCHONGEA Kwa muhimili mwingine .Nilitegemea Mkuu Wa wilaya angewashauri wakulima wakate RUFAA badala ya kitendo cha KUCHONGEA alichokifanya.Je atakuwa anachongea kila kesi ambayo mkulima anashindwa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app