DC Gondwe: Msaada wako mto Kawe. Watoto awaendi shule

DC Gondwe: Msaada wako mto Kawe. Watoto awaendi shule

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
MH DC
SHALOM
Tunaomba msaada wako wachimba mchanga mto Kawe wanachimba tope.

Watoto wanashindwa kwenda mashulen. Polisi Kawe wameshindwa kutusaidia wanakuja kukusanya pesa kila siku badala ya kuzuia malori

Tunaomba tusisubiri kusikia wamekufa watoto tunaomba marufuku kuchimba mto Kawe

Wako
Wananchi wa makazi mapya
Kawe
 
Mpwa kilio chako hiki ni cha siku nyingi sana, bado hakijapata ufumbuzi
Aise,hivi kituo kile K bado kinaendeleza dili tu

Ova
 
Wakiacha chimba mto unajaa mchanga, serikali ndiyo imeruhusu, hata Jangwani serikali ndiyo imeruhu wachime
 
Wakiacha chimba mto unajaa mchanga, serikali ndiyo imeruhusu, hata Jangwani serikali ndiyo imeruhu wachime
Wiki 3 zilizopita nilisikiliza kisa Cha huu mto Kawe na wakazi wake, changamoto hapa wanachimba Hadi baadhi ya nyumba zimekwisha bomoka (kuanguka kabisa) hivyo inabidi kusimama kwa muda ila wachimbaji hawataki Tena walimfurumusha mjumbe na mapanga baada ya kujaribu kuwazuia wasichimbe mchanga
 
Nilijua hii ishu ilishashughulikiwa, poleni
 
Wiki 3 zilizopita nilisikiliza kisa Cha huu mto Kawe na wakazi wake, changamoto hapa wanachimba Hadi baadhi ya nyumba zimekwisha bomoka (kuanguka kabisa) hivyo inabidi kusimama kwa muda ila wachimbaji hawataki Tena walimfurumusha mjumbe na mapanga baada ya kujaribu kuwazuia wasichimbe mchanga
Police kawe watakuwa wanadakishwa hela hapo

Ova
 
Malalamiko aelekeze kwa Waziri wa mazingira, polisi moja ya genge la ulaji tu
 
Back
Top Bottom