Elections 2010 DC Igunga ni mkristo mkatoliki; Kwanini hajasema kitu?


Bakwata wanasema kuwa ni "mwanamke Muislam " kwa sababu mamlaka yao ipo kwenye Muislam. Tamwa na ndugu zake wao walipaswa kutetea mwanamke na CCM walipaswa kumtetea kama Mwana CCM.

Hapa kinachoonekana ni nani hodari wa propaganda tu.
Historia iliyowekwa kwanza licha ya kukosa ushahidi, haimaanishi kuwa kuvuliwa mtandio uliokwenda na nguo za kujistiri zisizobana sio vazi lililoamriwa kwa Waislam na pale Bi. Fatuma ameliwakilisha kuliko Waislam wengine au wenyewe.

Nafsi yangu ninawajua wanawake wengi walioolewa na Wakristo wakaendelea na dini zao na walipofika utuuzimani wakashika dini zaidi na kuvaa kama dini zao zinavyotaka ambapo hatua kubwa wanayofanya pia ni kujitenga makazi kimakazi na waume zao.

Kwa la huyu mama sijui, ila shamba la mumewe kufuga nguruwe au kuwa aliolewa na mkiristo hakumuondolei dini yake kama anayo. Naamini hakuna binaadamu aso dhambi kwa mujibu wa maamrisho ya dini afuatayo na angeamua kukaa chini angepata mengi ya kutafakari na kujutua

Pili hatujui Kama aliwathibitishia Bakwata kuwa yeye ni Muislam au la. Kwa vile Bakwata ni culprit wazoefu basi tunataka sana tuone na kwa hili pia waliokosea.Tunataka sasa atoe tamko rasmi kusema yeye ni Muislam. Kwangu huo nauona ni udhalilishaji wa aina nyengine kuwa sasa mtu alazimike kusimama mbele ya umma kulinda Imani yake!

Nadhani kimsingi hoja yako ingesimama vyema iwapo Bi Fatuma si Muislam na angesimama kupinga na kusema "yeye si Muislam" ili Bakwata iache kumtetea. Na ikiwa yeye ni Muislam hakuna lazima yoyote ya kusema hivyo kwa vile haki Yake tayari anaipata.

Sishabikii Bakwata kufikia kutoa matamko makali kiasi hiki, lkn haki ya kufanya hivyo wanayo kwa vile wanaemtetea anawakilisha Uislam.

Chadema did wrong kumvua mtu stara yake ambayo bila ya hiyo mwanamke Yule haamini kuwa kastirika. Purukushani ingetokea na wakamchanua blouse yake jee? Wangemtoa hivyo hivyo au wangemstiri? Ukosefu wa tact wameshindwa kuelewa kuwa mtandio na blouse una hadhi sawa kwa baadhi ya watumiaji. Na ikiwa jibu ni kuwa hata Kama angevuka blouse wangemtoa hivyo hivyo, I got nothing but to shake my head

(now hizi propaganda za JF aside mpaka zitakapoandikwa walau kwenye gazeti manake hapa mtu can say anything wala haombwi ushahidi na tunaamini kwa vile tu ni yenye kutupendeza)
 
Last edited by a moderator:
Reactions: EMT
haya ndo matatizo ya kudandia treni kwa mbele. Mwanasiasa ataonekana poa tu ila kiongozi wa dini ataonekana mchochezi, mpumbavu na mdini. Bakwata tutakeni radhi
 
Kwani Fatuma au Fatima ni jina la Kiislamu au la Kiarabu? inamaana waarabu wote ni waislamu? Mbona kuna waislamu waingereza wanaitwa John,Davis au Joseph na kama kumkamata huyo mama kumedhalilisha uislamu alikamatwa akihubiri Msikitini? acheni sheria ichukue mkondo wake msiingize mambo ya udini.
 
Mungnu hamfichi mnafiki na siku ya kufa nyani miti yoote huteleza. Haya mambo inawezekana ni ya kweli kwa sababu CCM mara zote ni mabingwa wa mazingaumbwe haswa kipindi cha uchaguzi. Mbaya zaidi viini mamcho vyao ni vya kitoto kila mtu anavishtukia na hapa tujiandae kuvunjika tena mbavu kwa vionja lukuki
 
lakini hakuna mahali aliposema kuwa yeye ni muisilamu, alicholalamika ni kuachwa uchi! Sasa hiyo ya kuwa muisilamu mnaitoa wapi?

hehehehe heheheheh heheh hahahah hahahahh hahahahaha. Duuu msiniumize mbavu vigeugeu
 
BAKWATA mtaweka wapi nyuso zenu? Ama kweli njaa ni NOMAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huyu mama ni CCM.

Nafikiri atasema ukweli baada ya uchaguzi.

Wacha CCM waendelee kulitumia hili swala kama Mtaji wao Kwanza kwasababu hawana Sera kwa wananchi.

Yaani Nyie CCM badala ya kupiga Kampeni kwa kuwaambia Igunga Mtawafanyia mambo gani ya Kimaendeleo mnaona muongelee mambo ya kuvuana hijabu.

Hivi nyie wana igunga Hili la kuvuana Hijabu linawasaidia nini?
 
Mimi naishi mbezi beach karibu kabisa na kanisa la Bikira maria mama wa Huruma. Huyu mama Fatuma Kimario huwa namuona kanisani mara nyingi tu. Hata kwenye zamu za kusimamia kanisani siku za Jumapili ambazo hupangwa kijumuiya huwa namuona anasimamia. Infact nimeshangaa kusikia kuwa anaitwa Fatuma na ni muislamu. Anyway, huenda kabadili dini, lakini ukweli ni kuwa huwa anasali kanisani kwetu Bikira Maria mama wa Huruma.
 


Mkuu nadhani utakuwa umesahau au hujui kabisa. Ndoa za mchanganyiko zipo kwenye ofice ya dc. Kanisani kuna ndoa za wakristu tu! Kama kuna m1 ambaye ni wa dhehebu lingine, hata kama ni la kikristu ni lazima abatizwe na awe muumini wa hilo kanisa ndio ndoa ifungwe. Kama ni wa dini nyingine ndio anapata mafundisho ya dini kwanza.
Sijui ndugu zangu Waislam!
 
huyu mama kwa kukaa kimya hakika anastahili adhabu kubwa
Nachoweza kusema Fatuma si mkristo wala muislam bali dini yake ni VUNIA TUMBO
 
duh,hap tatizo lipo!kweli ndani ya nchii hii,akili ya mbayuwayu changanya na yako....
 
yupo jumuiya ipi?
 
Jina sio hoja, SHAME on BAKWATA


Nikuelimishe tu kidogo; si lazima kwa mwislamu kubadilisha jina pale anapobatizwa. Vile vile majina kama Fatma si majina ya kiislamu bali kiarabu ba kuna waarabu ambao ni wakristu, majina kama Petronella sio ya wakristu bali ni ya wazungu na kuna wazungu waislamu.
 

Kwa uelewa wangu kuhusu dhehebu la roman catholic huwa hawafungishi ndoa kama wewe sio muuminiwa catholic hata kama ulikuwa anglikani ama lutherani unapewa mafunzo yao ndipo unafungishwa ndoa, na kama ni muslim anaolewa na mkristo lazima anapewa mafundisho ya ubatizo na kipaimara ndipo ndoa inafungwa bila hivyo ndoa haifungwi.
 
Hata mke wa PM alikuwa muisilamu, amebatizwa hapo St. Peter's kwa jina na Petronela, wala si Tunu tena!

walete walete hao nasikia wako wengi tu hata mama etu anaitwa salome badala ya salma
kabatizwa kigango cha mpiji nusu mkata
 
Si kila mwenye koti jeupe ni daktari, wengine wauza nyama buchani.
..Mkuu umenikumbusha tukio moja binti yangu wa miaka 2.1/2 kila anapopelekwa hospitali nadhani alikuwa anakutana na madaktari wanaovaa makoti meupe na yeye akajenga akilini mwake kuwa kila anayemuona na koti jeupe anajua ni daktari. Kuna siku amepita na mama yake mwenge pale wakati bibie anatafuta parking ya gari akatokea muuza nyama pale ambaye tumezoea mara kwa mara kununua minofu kwenye bucha yake anamuelekeza wife parking nzuri huku akimuwahi mteja wake wasimvamie wenyee bucha wengine. Kwa nini mtoto asipige kelele eti mama yule wa kuchoma sindano anakuja tuondoke......Leo umenikumbusha hicho kituko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…