Yeye kama si Muislam alitakiwa afike aseme yeye si Muislam. Kama yeye ni Muislam hana haja ya kwenda kwenye vyombo vya umma kujieleza kuwa yeye ni Muislam, kwa sababu tutataka afanye hivyo kwa faida ya nani? Kama haki yake ya kutetewa kama Muislam tayari ameshaipata. Kwangu inanishangaza kweli kweli kuwa tunataka "mama huyu adai kuwa yeye ni Muislam". Afanye hivyo ili iweje?

Besides hatujui kuwa alizungumza na Bakwata kabla au la. Kwa mujibu wa Video iliyowekwa hapo juu, Bakwata wanazungumzia kuwa aliambiwa "unajifanya Hajat....." kabla ya kuvuliwa mtandio wake. Tuamini kuwa Bakwata imeongeza chumvi, wanachadema hawakumwambia hivyo, lakini kuna elements zinazoonyesha kuwa walijiridhisha kuwa ni Muislam au wamemuona akitekeleza dini yake zaidi ya kuvaa huo mtandio (Usikute pengine ni Hajat kweli).

Chadema did wrong, awe huyo mama ni Muislam au la (Naamini ni Muislam hadi pale vyombo vya habari vitakaposema vyenginevyo, na sio propaganda za JF zisizoombwa ushahidi zinazoletwa na wana Chadema). Kumvua mtu nguo yake anayoamini kuwa ni stara kwake ni kosa. Iwe nguo hiyo ni Mtandio, Blouse, skirt au nyengineyo yoyote. Kilichotokea ni udhalilishaji wa wazi kwa mwanamke. Hatukemei sasa kwa vile aliyefanyiwa ni CCM lakini itatu cost baadae kukiacha chama cha siasa kuchukua sheria mkononi zinazoambatana na udhalilishaji.