DC Ikungi awapeleka watatu TAKUKURU kukwamisha ujenzi kituo cha afya Irisya wamaliza milioni 500 ujenzi haujakamilika

DC Ikungi awapeleka watatu TAKUKURU kukwamisha ujenzi kituo cha afya Irisya wamaliza milioni 500 ujenzi haujakamilika

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 01/11/2022 amemuelekeza mkuu wa takukuru wilaya ya Ikungi kuanza uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watumishi watatu waliokuwa wanasimamia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Irisya tarafa ya Sepuka jimbo la singida magharibi

Pamoja na hatua hiyo pia amemuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Mhe. Justice Lawrance kupeleka team ya uchunguzi ambayo itakuwa na lengo la kuchunguzi mienendo ya tabia za watumishi hao watatu ili pia waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi za halmashauri

Dc Muro amesema hatua hiyo imekuja baada ya mradi huo kukwama mara mbili kumalizika uku kiasi cha shilingi milioni 500 kikiwa kimeshatumika chote pasipo mradi kukamilika hatua iliyosababisha mradi kukwama kumalizika kwa miezi mitatu zaidi

Dc Muro amesema walivyofika kwa nje unaweza kuona kazi imeisha ila ukiingia ndani utabaini maabara haijakamilika, vyoo vyote vya majengo yote havijakamilika, tiles za chini hazijakamilika, jengo la mochwari ndani halijakamilika, vyoo havijafungwa vyote na masinki ya kunawia mikono hayajakamilika, uku baadhi ya majengo yakiwa tayari na nyufa kitu ambacho hakiweza kufumbiwa macho

Katika hatua ingine ya kushangaza ni kitendo cha wasimamizi wa mradi huo kuita fundi ambae alitengeneza kipande cha ngazi za kupandia jengo la mama na mtoto na kisha kutoweka uku wakijua kuna ziara ya mkuu wa wilaya na walipoulizwa iweje walete fundi siku moja kabla na kwanini fundi huyo leo hakuwepo viongozi wote walikana kumuita na kumtambua fundi huyo uku wakijua kuna kazi imefanywa kwa siku moja tu

Dc Muro pia ametoa maagizo ya kukamilika kwa vituo vyote vya afya ambavyo vinajengwa na hela zikiwa zote zimeshatumika na kusisitiza wasimamizi wa vituo vya afya vya Iyumbu, Ntuntu na iglanson kuwa tayari kwa lolote lile

"Wananchi hawataki kusikia malumbano yenu kwenye ujenzi wao wanataka kuona hela zilizotolewa na Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan zinatumika ipasavyo na miradi inamalizika pasipo visingizio " ameongeza Muro.

Tazama picha za ziara 👇🏾👇🏾

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi
01/11/2022
 

Attachments

  • IMG-20221101-WA0111.jpg
    IMG-20221101-WA0111.jpg
    69.2 KB · Views: 8
  • IMG-20221101-WA0112.jpg
    IMG-20221101-WA0112.jpg
    63.8 KB · Views: 9
  • IMG-20221101-WA0113.jpg
    IMG-20221101-WA0113.jpg
    45.6 KB · Views: 9
  • IMG-20221101-WA0107.jpg
    IMG-20221101-WA0107.jpg
    57.5 KB · Views: 8
  • IMG-20221101-WA0108.jpg
    IMG-20221101-WA0108.jpg
    45.9 KB · Views: 7
  • IMG-20221101-WA0109.jpg
    IMG-20221101-WA0109.jpg
    68.3 KB · Views: 7
  • IMG-20221101-WA0110.jpg
    IMG-20221101-WA0110.jpg
    73.4 KB · Views: 7
  • IMG-20221101-WA0105.jpg
    IMG-20221101-WA0105.jpg
    38.5 KB · Views: 7
  • IMG-20221101-WA0106.jpg
    IMG-20221101-WA0106.jpg
    27.1 KB · Views: 7
  • IMG-20221101-WA0104.jpg
    IMG-20221101-WA0104.jpg
    41 KB · Views: 8
  • IMG-20221101-WA0103.jpg
    IMG-20221101-WA0103.jpg
    46.2 KB · Views: 8
ukoo wa panya tenda wanapeana wao kwa wao ndiyo maana kazi haziendi wanawaza wizi
 
Back
Top Bottom