Nimeipata mahali hii, [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Namfahamu Sana wakili msomi mzee Merinyo, watoto wake lengai na lesi. Familia hii ni wastaarabu Sana. Wapole na wanajiheshimu.
Napata ugumu Sana kuskia eti hawa vijana wanatumia Elimu yao ya uwakili kunyanyasa watu wakati Nina uhakika hapa Arusha mjini wao wamekua wakisaidia watu sana mno. Ni kimbilio la wananchi wengi, wametumia taaluma yao vizuri kusaidia kupatikana kwa Suluhu na haki za wananchi wengi Sana.
Nakumbuka wakili msomi Lengai pia aliwahi kuwa wakili kule lhrc. Amewatumikia wananchi wa mkoa wa Arusha kwa moyo na kwa uaminifu mkubwa sana.
Nikiwa kama mwananchi wa kawaida, natoa Rai kwa viongozi haswa hawa madc, kutumia mamlaka yao vyema. Ni kweli wanaruhusiwa kuweka watu ndani masaa 48, lakini nawasihi Sana wasionee watu. Wasiwavunjie watu heshima. Wajali utu wa watu. Hata kama wewe ni dc haikupi mamlaka ya kutumia ubabe na wakati mwingine kuvunja Sheria kiholela.
Siaminini Mh.dc Jerry muro alikua mwenyewe mpaka aakavamiwa na kushambuliwa na hao mawakili wawili, sio kweli. Ziara kama hiyo hapo ni lazma dc alkua na watu, kwanini waliacha dc akavamiwa???
Mkifika mahali enyi madc ulizieni historia za watu kwanza. Sio mnakomoa watu kwa interests zenu. Ofisi zenu zinatumika kuonea watu wakati mwingine. Haki za watu zinapokwa. Mtu Ana haki nyie mnapotezea haki za watu, Tena mnatweza utu wa watu, na kushusha heshima za watu.
Mmepewa hayo madaraka kama dhamana ili kutumikia wananchi, tendeni haki. Na mumsaidie Mheshimiwa Raisi ambae Ana Nia thabiti ya kuingoza nchi hii kwa haki. Msimwangushe kwa kuleta migogoro juu ya migogoro.
Pia nashauri SERKALI ifikirie kuchagua wakuu wa wilaya wanaotoka sehemu husika sababu wanaelewa mazingira vizuri na watu wa hayo maeneo.
Nasikitika Sana Sana kwa haya yaliyotokea.
Mama Ngina-Arusha.
Sent from my Infinix X653 using
JamiiForums mobile app