DC Jokate Mwegelo: Taa za kisasa kuwekwa eneo la nje mkabala na uwanja wa Benjamin Mkapa (Temeke)


Nilisikia betri zinakaa mbili. Moja ni 500,000×2=1,000,000

Ni maneno ya vijiweni sijui kama yana ukweli.
 
Ufundi?

material zingine?

vibarua?
Injinia soma hiyo
 
Wananchi wanahitaji maendeleo mbinu za kurejesha hela mifukoni muonekano wa ofisi hauna maana yote kwa nchi maskini kama Tz, huyu bint anapenda starehe anashindwa kufahamu anatakiwa kuwa field muda mwingi sio kukaa ofisini na kusuka suka miguu kwenye viti vya kuzunguka na AC.,

Ofisi ya mkuu wa Wilaya inatosha meza 1 na kiti cha mbao kimoja na vyengine 3 ata vya plastic ili ikitokezea akiwa ofisini akipata mgeni asikae chini inatosha kabisa.

Yeye anataka akae ofisini kama nyumbani kwake. taa nje zinawaka ndani AC zinapiga kelele
 
Na hiki ndio kipaumbele ?, Taswira ?

Ingekuwa bora kwanza angebuni namna ya kupata hizo chenji sio kuchukua zilizopo, nina uhakika ana lobbying power kubwa
 
Jokate Mungu amsaidie nahisi kama mzigo aliyopewa ni mzito kuliko umri wake

Maana mabingwa wa kutafuna miradi ya maendeleo wapo temeke asipo kuwa makini watamjaza upepo ili waendelee kupiga



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taa zenye mwanga mkali zinaenda hadi shilingi milioni mbili na zaidi, inategemea wameainisha taa zenye nguvu kiasi gani!
 
lakini tumeambiwa wanarekebisha uchumi kwanza na kuvutia uwekezaji labda pengine wawekezaji wakishakuja hapo baadae ndo gharama inaweza ikapungua
 
Yuko vizuri kichwani!
Hamna kitu hapo! Wilaya za TZ unaweza ukaanza na kupamba eneo la ofisi? Temeke ina matatizo ya shule utadhani siyo mjini. Mpaka leo shule za msingi watoto wanapitia madirishani na sakafu za vumbi. Ni vi mtu vinavyosifiwa kwa mengine tu!
 
Halafu hizo taa baada ya wiki 2 ni mwendo wa hii inawaka,ile haiwaki,hii inasinzia sinzia,nyingine imeegemea kushoto,nyingine imeegemea kulia...
 
Huku Buza kwa Lulenge atakuja lini kwani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…