Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa akiingia katika mfumo wa Centralized GOT-HOMIS ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mfumo huo wa matibabu katika vituo vyote vya huduma za Afya vinavyomilikiwa na serikali.
Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 17/03/2025 katika kituo Cha Afya Songe na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mh Mgandilwa alitoa miezi 3 kwa vituo vyote kuwa vimegunga mfumo huo.
Mfumo huo wa matibabu unarahisisha huduma za matibabu na kuweka kumbukumbu za mgonjwa ambazo zinaweza kuonekana katika vituo vingine vya Afya sanjari.