GE2025 DC Kissa: Kipindi hiki cha Uchaguzi tutawatumia Mgambo kutazama Usalama

GE2025 DC Kissa: Kipindi hiki cha Uchaguzi tutawatumia Mgambo kutazama Usalama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mkuu wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe Kissa Kasongwa amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kwenda kuwa wazalendo na nchi yao na kuilinda kwa wivu mkubwa ambapo pia ametoa ahadi ya serikali kuwatumia kwa ajili ya kutazama usalama katika kipindi cha uchaguzi.

DC Kissa ameeleza hayo wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu kwa vijana zaidi ya 50 wa kata ya Tandala wilayani humo walionufaika na ujuzi mbalimbali ikiwemo kwata, mapigano, kulenga shabaha, usalama wa raia yaliyowaweka kuwa na ukakamavu katika kukabiliana na mazingira yao.

"Tukajitokeze kuchagua viongozi tunaowahitaji kwasababu uchaguzi ndiyo unaamua hatma ya maendeleo, na vijana ambao mmehitimu leo niwape taarifa kwamba kipindi cha uchaguzi tutawatumia kutazama usalama", amesema DC Kissa.

Aidha Kissa amesema kupitia mafunzo hayo taifa limeongeza vijana wenye nidhamu na wenye uzalendo wa kweli kwa taifa lao na kutoa pongezi kwa vijana hao kwa kujitoa.

Awali wakitoa shukrani vijana hao akiwemo Petro Luvanda wanasema kupitia mafunzo hayo wataweza kufanya kazi kwa pamoja huku pia wakiiomba serikali kuwafikiria kwenye fursa mbalimbali ikiwemo kwenye mikopo ya halmashauri jambo ambalo limepokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo.

 
amani ndio msingi wa maendelea naunga mkono mgambo nao kuongeza nguvu kipindi hiki
 
Awa mgambo wapewe elimu ya kutosha sio kuvunja meza za wamachinga tu
 
Back
Top Bottom